Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 179 2025-04-29

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuvifanya vivutio vya Mapango ya Nang’oma, Namaingo, Likolongomba na Nampombo kuwa na tija kwa Taifa?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imeanza kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vivutio vya Mapango ya Nang’oma, Namaingo, Likolongomba na Nampombo vinakuwa na tija katika uchumi na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha Adhimisho la Kumbukizi ya Vita ya Majimaji ambalo hufanyika Mwezi Agosti kila mwaka katika Wilaya ya Kilwa kwa lengo la kutangaza vivutio mbalimbali vya kilwa ikiwemo mapango hayo kwa wadau wa utalii, washiriki, waandishi wa habari na wananchi wanaotembelea katika tukio hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matarajio ya Wizara ni kuwa jitihada zinazoendelea zitaongeza idadi ya watalii na wageni wanaotembelea maeneo hayo. Hivyo, Wizara inatoa rai kwa wadau wa sekta ya utalii kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye shughuli na huduma za utalii katika maeneo haya. Lengo ni kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa wananchi wa Kilwa na Taifa kwa ujumla. (Makofi)