Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuvifanya vivutio vya Mapango ya Nang’oma, Namaingo, Likolongomba na Nampombo kuwa na tija kwa Taifa?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Awali ya yote nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kiasi kikubwa chenye tija katika sekta yetu ya utalii. Ikiwemo kutoa GN ya Kumbukumbuzi ya Vita vya Majimaji kwa Mnara wa Majimaji pale Nandete kupitia GN namba 166 na GN namba 163 ambayo inatambua hayo mapango mawili yaliyoelezwa kwenye …
MWENYEKITI: Swali lako.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata pia boti ambayo imeongeza watalii mara dufu kule Ukanda wa Pwani wa Kilwa. Swali langu la kwanza; ni mwaka 2024 wakati wa maadhimisho ya vita vya majimaji Serikali iliahidi kwamba itajenga jengo la makumbusho pale Nandete na kujenga ngazi za kushukia katika Pango la Nang’oma. Je, mkakati huu umefikia wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ni kwamba, bado kuna maeneo mbalimbali ya vivutio vya majimaji hayajaendelezwa na kupatiwa GN. Kwa mfano kule alipokuwa anaishi Jemedari Kinjekitile Ngwale ambaye alikuwa ni mwanafalsafa na mhamasishaji wa vita ile, lakini pia kuna baadhi ya mapango bado hayajapata GN. Je, ni lini Serikali itatoa GN kwa hivyo vivutio vilivyobaki? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Wizara iliahidi kufanya ujenzi katika eneo lile kwa kuweka kituo cha utalii, lakini kujenga njia za kwenda kwenye mapango. Ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari Wizara imejipanga kwa ajili ya kukamilisha jambo hilo, tumekwishatenga bajeti ya kutekeleza miradi hiyo, kazi inayoendelea sasa ni kukamilisha michoro ya majengo hayo ili kazi iweze kufanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake la pili kuhusiana na GN kwenye yale mapango mawili yaliyobakia, lakini vilevile kwenye makazi ambayo Kinjekitile alikuwa akiishi. Ninataka nimhakikishie kwamba sasa hivi zipo kazi za kukusanya takwimu na taarifa za kiuhifadhi na kiutalii za maeneo hayo, kazi hii ikikamilika tunaamini kwamba ikifika mwaka 2026, tangazo hili la maeneo haya litakuwa limetoka. (Makofi)
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuvifanya vivutio vya Mapango ya Nang’oma, Namaingo, Likolongomba na Nampombo kuwa na tija kwa Taifa?
Supplementary Question 2
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nifahamu, Serikali imefikia hatua ipi kulipa fidia wakazi wa Kijiji cha Ndolezi kwa ajili ya kupisha uhifadhi wa kimondo katika Wilaya ya Mbozi?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Neema kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na taratibu za uhakiki wa jambo hili na mara baada ya kazi hiyo ikikamilika wananchi wale watapewa fidia yao.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved