Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 14 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 181 2025-04-29

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:-

Je, Serikali inachukua hatua gani na madhubuti kuhakikisha kunakuwa na ushindani kwa wafanyabiashara katika ununuzi wa pamba?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ununuzi wa pamba nchini hufanyika kwa utaratibu wa soko huru ambapo zaidi ya kampuni 35 zimesajiliwa na kupewa leseni ya kununua pamba na usajili unaendelea ili kuongeza ushindani. Kampuni hizi hununua pamba kulingana na hali ya soko ya msimu husika na bei dira iliyokubaliwa na wadau. Aidha, Serikali husimamia na kuhakikisha bei dira iliyokubalika na wadau inazingatiwa katika ununuzi wa pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na utaratibu huo, Bodi ya Pamba imeingia mikataba na Kampuni za ununuzi wa pamba ambao wameajiri Maafisa Ugani wanaotoa huduma za ugani katika kata zinazozalisha pamba kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo. Kampuni hizo zinapewa leseni ya kununua pamba katika kata zilizoajiri Maafisa Ugani kulingana na bei dira inayokubaliwa na wadau kwa msimu husika kulingana na bei ya soko. (Makofi)