Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Je, Serikali inachukua hatua gani na madhubuti kuhakikisha kunakuwa na ushindani kwa wafanyabiashara katika ununuzi wa pamba?

Supplementary Question 1

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mfumo wa sasa wa AMCOS kupokea fedha kutoka kwenye kampuni, ndipo AMCOS inunue pamba kwa niaba ya hizo kampuni hauruhusu kabisa ushindani na kwa kuwa Wizara mlifanya utafiti kidogo mkaona huo utaratibu una kasoro; ni kwa nini Serikali isiruhusu Mfumo wa “Simiyu Model” wa kuwaruhusu wanunuzi ama kampuni za pamba kuwa kila mmoja na mlango wake wa kununulia pamba ili kuruhusu huu ushindani wa kweli na halisia? Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Mashimba Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi kwani amekuwa ni mdau mkubwa katika zao la pamba na amekuwa akilifuatilia kwa ukaribu mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kimoja ambacho nimthibitishie, hili alilolizungumzia yeye kama Mbunge tumeshalipokea katika ofisi yetu na kesho tarehe 30 Aprili, tutakuwa na Mkutano mkubwa wa Wadau pale Shinyanga ambapo katika moja ya jambo litakalojadiliwa ni pamoja na haya mapungufu ambayo ameyaeleza na namna bora ya kutumia Mfumo wa “Simiyu Model” katika ununuzi wa pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya tarehe 30 (kesho) tutaweka utaratibu mzuri ambao ninaamini utakuwa na faida kwa wadau wote wa Sekta ya Pamba. Kwa hiyo, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge hili tumelizingatia na kesho tutapata majibu yake ya mwisho. (Makofi)