Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 43 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 550 | 2025-06-10 |
Name
Esther Edwin Maleko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu unatokea katika sekta nyingi nchini. Ili kudhibiti uharibifu huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandaa sera, sheria, kanuni, mikakati na miongozo mbalimbali inayobainisha hatua zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto hizo. Hii inajumuisha Sera ya Taifa ya Uhifadhi wa Mazingira ya mwaka 2021, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191 ikisomwa pamoja na Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Namba 5 ya mwaka 2025, na Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira wa mwaka 2022 – 2032.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa mazingira na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kupitia njia mbalimbali, ikiwemo pamoja na vyombo vya habari, ziara za viongozi na mafunzo shuleni, nakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved