Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu?
Supplementary Question 1
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa pamoja na juhudi zote hizo za Serikali bado uharibifu ni mkubwa sana wa mazingira; je, Serikali imefanya tathmini gani kuona sasa ni wakati mwafaka kabisa kuleta ufanisi katika sheria hizo na sera ambazo ziko zimeshapangwa kama alivyoeleza kwenye jibu la msingi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mlima Kilimanjaro ni kivutio kikubwa sana na kinaingiza hela nyingi nchini. Mlima huo, kivutio hicho ni kwa ajili ya theluji iliyo juu ya mlima ulio chini ya equator. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha theluji ile haimaliziki kuyeyuka? (Makofi)
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza Mheshimiwa Malleko, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyoeleza katika jibu letu la msingi kwamba moja miongoni mwa njia ambazo tumezitumia ama tunaendelea kuhakikisha kwamba tunadhibiti athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi kama tulivyoeleza kwamba tuna sheria, tuna miongozo, tuna kanuni, na tunazo kampeni mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie Mheshimiwa, ndani ya sheria hizi, ndani ya miongozo hii, ndani ya kanuni hizi, ndani yake mna maelekezo ya kampeni mbalimbali zikiwemo kampeni za utunzani wa vyanzo vya maji, zikiwemo kampeni za upandaji wa miti, zikiwemo kampeni za matumizi ya nishati safi ya kupikia, lakini zikiwemo kampeni za utoaji wa elimu kwa wananchi, lakini zikiwemo kampeni za kuendelea kutafuta fedha ili lengo na madhumuni tuhakikishe kwamba tunapambana kwa vitendo dhidi ya athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo la athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi Serikali haijalinyamazia kimya na hatua zilichukuliwa, zinachukuliwa na zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ipo mikakati mbalimbali ambayo kama Serikali tumechukua katika kuhakikisha kwamba tunadhibiti hali ya mmomonyoko ama hali ya uyeyukaji wa theluji ama barafu katika Mlima Kilimanjaro. Sisi Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na KINAPA tumechukua hatua madhubuti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza hivi karibuni tulishiriki mkutano mkubwa wa Kimataifa, ulifanyika pale Tajikistan. Ulikuwa unazungumzia masuala ya Glaciers' Conservation, namna ambavyo tutahifadhi barafu na theluji kwa zile nchi ambazo zina milima yenye barafu duniani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mambo mengine tulikubaliana kwa kauli moja, hatua ya kwanza twende tukadhibiti matumizi ama shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika milima hiyo, lakini tulikubaliana twende tukatafute fedha, kwa sababu tunaamini haya yote yatafanyika baada ya kupata fedha ndiyo tunakwenda kuhifadhi milima yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tulikubaliana kwamba tukapande miti ya kutosha, lakini tuwahimize wananchi wa nchi husika waache kuchoma moto na kufanya shughuli nyingine ambazo kwa namna moja zitapelekea uharibifu na kupungua kwa theluji katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Name
Asya Mwadini Mohammed
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu?
Supplementary Question 2
MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwepo na uchafuzi wa kimazingira katika kingo za bahari na mito, na ukizingatia fukwe hizi za bahari tunazitegemea sana kwenye masuala mazima ya kuhamasisha utalii ndani ya Taifa letu, imekuwa ni sehemu ya kuleta mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kingo hizo za bahari uchafu unavyoenda baharini pia unapelekea madhara mbalimbali ndani ya bahari na kupelekea maradhi mbalimbali. Nini mkakati wa Serikali wa kuzisimamia fukwe hizi na kuzisimamia vizuri ili kuweza kuyatunza mazingira hayo? (Makofi)
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Asya, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna baadhi ya shughuli zinafanyika katika kingo za bahari lakini sio tu kwenye kingo za bahari hata kwenye kingo za mito, kingo za maziwa ambazo ni sehemu muhimu ya vyanzo vya maji vinavyosaidia shughuli nyingi za kiuchumi na mambo mengine katika nchi yetu na shughuli hizi zinapelekea kuchafua baadhi ya maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti sasa zipo hatua ambazo kama Serikali tumezichukua; kwanza ni kusimamia sheria, hilo ndilo la kwanza, kwa sababu watu wengi wanafahamu kwamba kutupa taka maeneo hayo ama kufanya uchafuzi ni moja miongoni mwa makosa. Sasa sisi kama Serikali tumeendelea kusimamia sheria, sheria inayosimamia mazingira hasa mazingira ya pembezoni mwa vyanzo vya maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumekuwa tunaendelea kutoa elimu kupitia makongamano, kupitia washa lakini kupitia shughuli mbalimbali za kimazingira, lakini kikubwa zaidi tumeendelea kusisitiza wananchi, kwamba shughuli zinazofanyika katika maeneo haya ya fukwe zisiharibu mazingira, kwa sababu mazingira yetu ndio kitu pekee ambacho tunakitegemea, nakushukuru.
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu?
Supplementary Question 3
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kutokana na mabadiliko ya tabianchi Mto Mbulumi umekuwa ukileta athari kubwa sana kila mwaka katika Vijiji vya Kilimanjaro, Kichangani, Dunduma na Kisala na vijiji hivi vipo kwenye hatari ya kupotea kabisa, je, nini mkakati wa Serikali katika kuudhibiti huu mto ili usiendelee kuleta atharai katika hivi vijiji?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayoifanya, kwa kweli kila anaponikuta lazima aniambie changamoto hii kiasi kwamba kuonesha kwamba wananchi imekuwa ni changamoto kubwa, lakini ni kweli kwamba tumeshakaa na Mheshimiwa Mbunge, tumeshazungumza na kuna kipindi alikuja na Madiwani wake tukakaa tukazungumza Madiwani wenye kata hizo na vijiji hivyo. Of course jambo hili ni jambo ambalo limewagusa wananchi wa maeneo hayo, nimwambie Mheshimiwa kwamba tayari Serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kujenga kuta na kushughulikia changamoto zote ambazo aidha mito ama bahari, ama maziwa maji yanaingia kwa wananchi yanakuja kuleta changamoto, lakini kubwa nimwambie Mheshimiwa kwamba kama tulivyopanga, tulivyokubaliana kabla Bunge hili halijamaliza basi tutaona namna ya kwenda na kukaa na kuzungumza na wananchi kuona namna ambavyo tunaweza kuwasaidia, nakushukuru.
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Vijijini
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu?
Supplementary Question 4
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ni kinara wa utunzaji wa misitu inayovunwa hewa ya ukaa, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia hawa wananchi wa Wilaya ya Tanganyika ambao wamevuna tani za carbon ambazo hazina mnunuzi?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kakoso kutoka Wilaya ya Tanganyika kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii niwashukuru na kuwapongeza sana Wilaya ya Tanganyika na wilaya nyingine kwa kuwa wameitikia wito wa Serikali wa kuendelea sasa kuitumi hii fursa ya kutunza misitu na kuweza kupata carbon ya kutosha ili tuweze kutengeneza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ikiwemo shule, kujenga barabara, kujenga maji na kujenga haspitali za kisasa.
Mheshimiwa moja ya miongoni mwa mkakati mkubwa wa Serikali hasa baada ya kuanzishwa kwa hii biashara ya carbon ni kuhakikisha kwamba tunawatafutia wananchi masoko ya kutosha na ya uhakika ya carbon hii. Tayari Serikali imeshawakaribisha makampuni mbalimbali kuja kuwekeza pamoja na kuiweza kununua na kuweza kupata fedha za kigeni za kuweza kusaidia. Nimwambie Mheshimiwa kwamba jambo hili lipo kwenye mchakato Serikali inalifanyia kazi, wakati utakapokuwa tayari tutaona namna ambavyo Serikali inaweza kuchangamkia fursa hii na wananchi wakanufaika, ninakushukuru.