Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 43 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 551 | 2025-06-10 |
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: -
Je, zipi athari za kisayansi zinazosababishwa na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa hapa nchini hakuna athari za kisayansi ambazo zimesababishwa na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, hii ni kwa sababu ufugaji unafanyika katika maeneo yanayokidhi vigezo vya kisheria na kitaalamu. Maeneo hayo yanabainishwa kwa utafiti na tathmini ya athari za mazingira na jamii inayofanywa na Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI). Vilevile wafugaji wa samaki kwa vizimba wanafundishwa jinsi ya kutumia mbinu bora za ufugaji wa samaki kwa vizimba ikiwa ni pamoja na matumizi ya chakula bora, vifaranga vya samaki wenye asili ya eneo husika na udhibiti wa magonjwa. Aidha, ufugaji wa samaki kwa vizimba umekuwa na mafanikio katika nchi kadhaa duniani hususani Misri, Uganda na Zambia ambapo umechangia kuongeza kwa uzalishaji samaki katika nchi hizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, iwapo ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba utafanyika bila kufuata taratibu, athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na uchafuzi wa mazingira na upotevu wa bioanuai za asili (genetic pollution). Hivyo, Wizara inaendelea kujenga uwezo wa kuwasimamia wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ili kuzingatia sheria, kanuni na miongozo kwa lengo la kuwa na ufugaji wenye tija, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved