Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Industries and Trade Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 552 2025-06-10

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. EDWIN E. SWALLE K.n.y. MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha eneo mahsusi la viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya misitu?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inakubaliana na dhana ya kuanzisha eneo mahsusi la viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya misitu kwa kuwa inaendana na mipango ya kuanzisha kongani ya viwanda ikiwa ni pamoja na mpango wa kuendeleza bidhaa za mbao zilizohandisiwa (Engineering Wood Product Framework, 2021-2031), lengo ni kuongeza thamani ya mazao ya misitu kwa kuzalisha bidhaa za mbao handisiwa kama vile veneer, plywood, marine board, blockboard na samani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali imeandaa Mpango Maalum wa Kuendeleza Viwanda unaotarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026. Kupitia mpango huo imepanga kuanzisha kongani za viwanda ngazi ya halmashauri nchini kulingana na rasilimali zinazopatikana katika halmashauri husika ikiwa ni pamoja na kongani ya viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya misitu.