Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Water and Irrigation Wizara ya Maji 553 2025-06-10

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:-

Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Serikali imeanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa dakio (intake) katika Bwawa la Milala lenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 13 kwa siku, ujenzi wa miundombinu ya kutibu maji (water treatment plant) yenye uwezo wa kutibu maji lita milioni 12 kwa siku, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 115 sanjari na ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 2,000,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 40% na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2025 na kunufaisha zaidi ya wananchi wapatao 245,764 waishio katika Manispaa ya Mpanda. (Makofi)