Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yake yenye kuleta tumaini. Mimi nataka aji-commit kabisa ni lini huo mradi utakwisha Mpanda wana shida ya maji sana? Hilo swali la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, pamoja na juhudi kubwa anazozifanya Mheshimiwa Jenista Mhagama wa Jimbo la Peramiho kuhakikisha Kijiji cha Mdunduwalo kinapata maji. Je, ni lini sasa maji yatakamilika pale Mdunduwalo? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nimshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Ntara kwa swali zuri, lakini pia majibu ya Serikali ni kutokana na majibu ya msingi mradi huu utakamilika mwezi Oktoba, 2025, lakini pia kwa upande wa suala la Mradi wa Mdunduwalo nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Ntara kwa kuendelea kushirikiana na Mheshimiwa Jenista Mhagama, Mbunge wa Peramiho kwa kuhakikisha kwamba wananchi wa Mdunduwalo wanapata maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua juhudi ambazo zinafanywa na Mheshimiwa Dkt. Ntara na mradi huu tayari umeshafikia 25% na mradi huu unagharimu takribani shilingi bilioni 1.3 ambao Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza Wizara ya Maji tupeleke kutokana na maombi ya Waheshimiwa Wabunge. Nimtoe hofu, wakandarasi wako site na wanaendelea na kazi, naamini kabisa kwamba utakamilika kwa wakati. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 2
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, wananchi wa Wilaya ya Kyerwa tuliambiwa vijiji 48 kwa zaidi ya miaka 60 ya uhuru waliahidiwa wataletewa maji vijiji 48 vikihusisha Kata za Nkwenda eneo la Lunyinya, Kimuli, Nyakatuntu, Kamuli na maeneo mengine. Una neno gani kwao ambao zaidi ya miaka 61 wanasubiri maji? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nimshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Anatropia kwa kazi nzuri kwa kuendelea kuwasema wananchi wa Kyerwa. Natambua kabisa kwamba lengo kuu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na falsafa ya Mama Samia kumtua mama ndoo kichwani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wakati anaingia madarakani ni vijiji takribani 6,000 na kitu ndio vilikuwa na maji na sasa kati ya vijiji 12,318 ni zaidi ya vijiji 10,650 sasa vinapata huduma ya majisafi na salama. Kwa hiyo, tunaamini kabisa kwamba maendeleo ni hatua kwa hatua na tayari tumeshafikia katika hatua nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu na vijiji hivi 48 tutaviweka kwenye mpango ili lengo kuu ni kuhakikisha kwamba wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana ili tuone namna mzuri zaidi ya kufikisha maji kwa haraka kwa wananchi wake. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Lipangala, Kata ya Mkongobaki kilikuwa miongoni mwa vijiji vilivyopangiwa kuchimbiwa visima vile vitano. Sasa Kijiji hiki cha Lipangala kipo juu sana kwenye mwinuko mkubwa kuliko vyanzo vya maji ambavyo viko chini sana. Kwa hiyo, suluhisho pekee ilikuwa ni kisima, sasa na pale mtambo ulienda haukufanikiwa kupata maji.
Je, nini maelekezo ya Wizara kwa wataalam ili waweze kukamilisha kisima kile wananchi wa Lipangala waweze kupata maji? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana namshukuru sana kaka yangu kwa kazi nzuri anayoifanya kwa wananchi wake wa Ludewa na hakika pia tunamshukuru sana kwa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Maji kutekeleza miradi ndani ya jimbo lake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa eneo la Kijiji cha Lipangala ni kweli kabisa kumekuwa na changamoto hiyo na mara nyingi tukikosa maji sehemu moja tunachohitaji ni kutafuta sehemu nyingine ambayo ina maji na tukatengeneza mtandao kufika katika eneo ambalo hatujapata maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Rais wetu ni kuhakikisha Watanzania wote haijalishi unaishi wapi lengo ni kwamba wapate huduma ya majisafi na salama. Nimtoe hofu na tunatoa maelekezo kwa wataalamu wetu watuletee taarifa na tuone nini tukakifanye pale, tutaelekeza fedha na wataenda kuhakikisha kwamba wanatatua changamoto ya pale ili wananchi wako wapate huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 4
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Mradi wa kimkakati wa Benki ya Dunia kutoka Mradi wa Solai kule Tarafa ya Nambis uliasisiwa kuanza kutekelezwa mwaka huu. Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza mradi huu kwa sasa?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Zacharia, Mbunge wa Mbulu Mjini kwa kuendelea kuwa mwakilishi anayetambua maana halisi ya uwakilishi wake wa Mbulu Mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa Serikali ilifanya feasibility study kwa mradi huo na tayari tulishakamilisha detailed design ambayo imetupatia cost ya mradi huo ambapo ni takribani shilingi bilioni 85 inahitaji, lakini mradi huo unaenda kutatua changamoto katika zaidi ya vijiji 30 vya Mbulu Mjini kwa Mheshimiwa Zacharia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuharakisha upatikanaji wa fedha hizi na tayari andiko hilo limeshakuja Wizarani na Wizara inafanya juhudi stahiki kuhakikisha kwamba mradi huo unaenda kuanza mara moja na wananchi wa vijiji hivyo takribani 30 wapate huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 5
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kulikuwepo na miradi ya maji ambayo ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais miradi ya Oldonyosambu ambayo yenye fluoride, Siwandeti, Tarakwa, Kiranyi na Kimnya ambayo ilitakiwa ikamilishwe kwa ajili ya wananchi kuondoa changamoto ya maji.
Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha miradi hiyo ili kuondoa shida na kero na adha ya maji kwa wananchi hao? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kama ambavyo amesema Mheshimiwa Mbunge na Serikali tunatambua hilo na status ya sasa namuomba Mheshimiwa Mbunge tukubaliane baada ya kutoka hapa niweze kufuatilia na niweze kumpatia majibu stahiki kwa ajili ya wananchi wake wa jimbo lake. Ahsante sana.
Name
Masache Njelu Kasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupa
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 6
MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, Chunya Mjini tupo kwenye Mradi wa Miji 28 lakini mpaka sasa hivi mradi huu wa maji haujaanza na wananchi wa Chunya wanachohitaji ni maji.
Je, ni upi mpango wa Serikali wa muda mfupi kuhakikisha kwamba tunaongeza upatikanaji wa maji hasa kupitia visima virefu? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Masache Kasaka, Mbunge mahiri kabisa kutoka Chunya na sisi Wizara Mheshimiwa Mbunge tumekuwa tukiwasiliana na amekuwa akisisitiza kuhusu hili na kwa maslahi ya wananchi wake mradi wa matokeo ya haraka ambao unaendelea kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2025, nikutoe hofu huu mradi unaenda kufufua visima ambavyo sasa ndio itakuwa suluhisho la muda mfupi wakati tukiwa tunasubiri Mradi wa Miji 28 utakapokamilika. Nimtoe hofu mradi huu utaenda kutatua changamoto ya muda mfupi. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Joseph Anania Tadayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanga
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa Wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala?
Supplementary Question 7
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, Serikali ya Awamu ya Sita imeipa Wilaya ya Mwanga zawadi kubwa sana ya Mradi wa Same – Mwanga – Korogwe. Sasa swali langu ni je, ni lini mradi huu utafika katika moja ya vijiji vikubwa vya Wilaya ya Mwanga, Kijiji cha Kifaru kilometa zisizozidi mbili kutoka mradi ulipoishia? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Anania, Mbunge wa Mwanga. Ni kweli kabisa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwekeza mradi mkubwa sana Same - Mwanga na tayari kwa phase ya kwanza umeshakamilika mpaka katika eneo la Kisangiro hapo maeneo yote yanapata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunafahamu kuna umbali wa kwenda katika Kijiji cha Kifaru, hiyo inakuja katika phase ya pili na katika phase ya pili kutokana na bajeti yetu ya mwaka unaokuja kuna takribani shilingi milioni 150 itahitajika kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunafikisha mradi huo katika Kijiji cha Kifaru. Nimtoe hofu, sisi tunaenda kuhakikisha kwamba utekelezaji huo unafanyika kwa haraka ili wananchi wa eneo la Kifaru wapate huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana. (Makofi)