Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 554 2025-06-10

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa skimu za umwagiliaji utaanza na kukamilika katika maeneo yote ya Wilaya ya Kalambo yaliyobainishwa kuwa na fursa za kilimo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, katika mwaka 2024/2025 Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo upembuzi yakinifu na usanifu wa Skimu za Ilimba, Mkowe, Santamaria, Sopa, Kamawe, Kasanga, Katete, Mtuntumbe, Kasitu, Tatanda, Mao, Katazi, Mnazi, Kaluko, Kilesha, Kambo, Kalembe, Ulumi na Katuka zenye ukubwa wa jumla ya hekta 21,300 zilizopo katika Wilaya ya Kalambo. Upembuzi wa skimu hizo unatarajiwa kukamilika mwaka 2025/2026 na kuanza taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi. Aidha, mradi wa Skimu ya Selengoma yenye ukubwa wa hekta 1,500 iliyopo katika Wilaya ya Kalambo upo katika hatua ya ununuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi.