Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini ujenzi wa skimu za umwagiliaji utaanza na kukamilika katika maeneo yote ya Wilaya ya Kalambo yaliyobainishwa kuwa na fursa za kilimo?

Supplementary Question 1

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, skimu ya umwagiliaji iliyopo Kijiji cha Ulumi, Kata Ulumi ujenzi wake haujakamilika; je, ni lini ujenzi wa skimu hii utakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, lini Skimu ya Umwagiliaji ya Taqwa iliyopo katika Wilaya ya Chemba itaanza?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Skimu ya Ulumi ilijengwa zamani bila kufuata zile taratibu za mkandarasi na sisi sasa hivi kupitia Tume ndio maana tunafanya usanifu upya ili tuanze kuijenga upya iweze kuendana na wakati na isiwe inaharibika kila wakati. Kwa hiyo, ndio kazi kubwa ambayo tunaifanya sasa hivi na tukimaliza tunaweka mkandarasi ambaye ataanza kuijenga upya kama ambavyo mchoro utakavyokuwa umeainisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Skimu ya Taqwa na yenyewe ni moja ya skimu ambazo zipo katika utekelezaji na nimthibitishie tu kwamba katika hatua tulizopo sasa za kutafuta mkandarasi akishakuwa amepatikana basi ujenzi wake utaanza mara moja. Ahsante. (Makofi)

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini ujenzi wa skimu za umwagiliaji utaanza na kukamilika katika maeneo yote ya Wilaya ya Kalambo yaliyobainishwa kuwa na fursa za kilimo?

Supplementary Question 2

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kalenga lina skimu zaidi ya 19 ambazo ni chakavu sana. Nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba skimu hizi zinakarabatiwa? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimuondoe shaka Mheshimiwa Tendega kwamba katika Jimbo la Kalenga hizo skimu zote 19 na zenyewe zinafanyiwa usanifu wa kina na upembuzi yakinifu na tukishakamilisha maana yake zitaanza kujengwa zote. Hayo ni maelekezo ambayo tulipewa na Mheshimiwa Rais. Kwa hiyo, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge zitafanyiwa kazi. (Makofi)

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini ujenzi wa skimu za umwagiliaji utaanza na kukamilika katika maeneo yote ya Wilaya ya Kalambo yaliyobainishwa kuwa na fursa za kilimo?

Supplementary Question 3

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Skimu ya Umwagiliaji ya Lyamalagwa, Kata ya Sigili, Jimbo la Bukene ni skimu kubwa sana ambayo itakapokamilika itagharimu karibu shilingi bilioni 29 na wananchi wanaisubiri kwa hamu kubwa sana, lakini mkandarasi amekuwa na speed ndogo sana.

Je, Serikali ina kauli gani kuhusu kumharakisha huyu mkandarasi ili aweze kukamilisha Skimu hii ya Lyamalagwa, Sigili ili wananchi waanze kunufaika na kilimo cha mpunga? (Makofi

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

, nimuondoe hofu Mheshimiwa Selemani Zedi wa Jimbo la Bukene kwamba skimu hiyo tayari ina mkandarasi ambaye yuko kazini, lakini bahati mbaya ni kwamba yuko slow na ninailekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwenda katika eneo hilo kumsukuma huyu mkandarasi, lakini kuhakikisha kuona ni changamoto gani inamfanya achelewe kufanya hiyo kazi. Kwa hiyo, haya ni maelekezo na ninayatoa hapa. Ahsante. (Makofi)