Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 555 2025-06-10

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, kwa nini tangu mwaka 2018 hadi leo MSD haijapeleka majokofu manne ya mochwari katika Kituo cha Afya Mugeta – Bunda?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 21 Februari, 2024 Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ilipeleka jokofu lenye uwezo wa kuhifadhi miili sita katika Kituo cha Afya Mugeta na hadi sasa jokofu hili linafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kununua na kusambaza vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya kulingana na upatikanaji wa fedha.