Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, kwa nini tangu mwaka 2018 hadi leo MSD haijapeleka majokofu manne ya mochwari katika Kituo cha Afya Mugeta – Bunda?

Supplementary Question 1

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa wakati Kituo cha Mugeta kinajengwa tulipewa mwongozo kwamba kituo kile kinajengwa kwa shilingi milioni 700; shilingi milioni 400 ya ujenzi na shilingi milioni 300 ya vifaa, na shilingi milioni 300 hiyo iende MSD sio kwamba ni hela ya kukopa wala ya kuomba, na mpaka sasa tumepokea vifaa vya shilingi milioni 161, vifaa tiba vya Kituo cha Mugeta, lakini bado shilingi milioni 139 ambazo tuliambiwa tunapewa x-ray na sasa ni lini hiyo x-ray ya Mugeta itaenda kwa shilingi milioni 139 iliyobaki MSD?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali ina mkakati gani sasa wa kumaliza Hospital ya Wilaya ya Butiama ya Bunda?

MWENYEKITI: Hebu, kisemeo chako kimezima.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza Hospitali ya Wilaya ya Bunda ya Mkama, mkakati gani wa Serikali wa kumaliza hiyo hospitali kwa sababu bado hali yake siyo nzuri?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kwa kweli amekuwa ni mpambanaji na wakati wote akizunguka Wizarani kuhakikisha fedha zinakwenda kwenye wilaya yake hiyo ya Bunda.

Kwanza nimwambie kwamba amesema kuna zaidi ya shilingi milioni 130 ambazo bado zipo MSD kwa ajili ya x-ray na nimwambie tu kwa sababu pale kwenye kile kituo kuna utaratibu sasa wa kutaka kujenga hilo jengo la x-ray, kwa hiyo jengo la x-ray likiisha basi na hizo fedha zitatumika kwa ajili ya kuleta x-ray ambayo inatakiwa kwenye eneo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali lake la pili kuhusu hospitali yake ya wilaya anajua yeye mwenyewe alifuatilia na mwezi wa 12 ziliingia shilingi milioni 980 na zimefanya kazi kumalizia yale majengo yaliyokuwepo na siyo muda mrefu halmashauri yake iliandikiwa wakapewa ceiling ya shilingi milioni 500 na wameshaainisha vipaumbele vyao na sio muda mrefu shilingi milioni 500 hiyo itaingia ili kuweza kumalizia majengo yaliyopo pale kwenye hospitali yake.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, kwa nini tangu mwaka 2018 hadi leo MSD haijapeleka majokofu manne ya mochwari katika Kituo cha Afya Mugeta – Bunda?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa utaratibu uliopo hivi sasa wa kupeleka dawa katika halmashauri zetu kutoka MSD unategemea fedha ambazo zinatoka halmashauri ili kuagiza hizo dawa; je, Serikali haioni sasa wakati umefika wa kuipatia mtaji wa kutosha MSD ili iweze kwenda na wakati katika kuagiza dawa na kupeleka dawa katika halmashauri zetu?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu tu swali zuri la Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kwamba tunatenga hapa shilingi milioni 200 ambazo ndiyo hizo zinakwenda kwenye halmashauri zetu na ndiyo zinazotumika kupeleka dawa, kununua dawa sasa kupeleka kwenye halmashauri zetu, lakini anazungumzia jambo la MSD kupata mtaji na mnajua hapa tayari MSD ilishapewa shilingi bilioni 100 kwa ajili ya mtaji na Serikali itaendelea kufanya hivyo na kuna namna ambavyo Serikali inafanya ili pia MSD iweze kukopa na kushirikiana na wadau mbalimbali kuweza kufikia hilo lengo.

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, kwa nini tangu mwaka 2018 hadi leo MSD haijapeleka majokofu manne ya mochwari katika Kituo cha Afya Mugeta – Bunda?

Supplementary Question 3

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Chuo cha Afya PSI kilichopo Iringa kimechakaa sana na majengo yaliyoanza kujengwa hayajamaliziwa, je, mna mpango gani wa kumalizia chuo kile?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni 187 kwa ajili ya ujenzi wa vituo mbalimbali kwenye hospitali zetu za mikoa, lakini pamoja na ukarabati wa vyuo vya kufundishia wataalam wetu, lakini pia kujenga vyuo vipya, nimwombe Mheshimiwa Mbunge tukimaliza hapa, tukae chini tuangalie katika hicho chuo chake, katika fedha kama chuo chake kimepangiwa ili niweze kumpa jibu halali kwamba kimepelekewa shilingi ngapi ili hapa nisije nikataja figure ambayo siyo sahihi.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: - Je, kwa nini tangu mwaka 2018 hadi leo MSD haijapeleka majokofu manne ya mochwari katika Kituo cha Afya Mugeta – Bunda?

Supplementary Question 4

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Hospitali ya Manyamanyama, Kituo cha Afya cha Manyamanyama, mwanzoni ilikuwa iwe Hospitali ya Wilaya ya Bunda kutokana na idadi kubwa ya huduma inayotoa mpaka kwenye wilaya za jirani kule.

Je, Serikali hamuoni kwamba kuna haja ya kuiongezea mgao wa vifaa tiba ili iweze kutoa huduma stahiki maana sasa hivi imeelemewa ukilinganisha na huduma inayoitoa, inapata vifaa tiba kidogo na dawa, lakini huduma inayoitoa ni kubwa mpaka kwenye wilaya za jirani?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu alichokiuliza Mheshimiwa Ester Bulaya kipo straight forward na ukweli ni kwamba inatakiwa upeleke dawa kulingana na mahitaji, lakini kulingana na idadi ya watu na huduma kituo chenyewe kinavyotoa.

Kwa hiyo nimuombe sasa tukija hapa tuwasiliane na Mganga Mkuu wa Wilaya halafu sasa atuletee idadi halafu tuanze process ya kuiongezea dawa na vitu vingine kwenye kituo hicho.