Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 556 2025-06-10

Name

Antipas Zeno Mngungusi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Malinyi

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: -

Je, kwa nini Serikali isijenge mitaro katika Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Namtumbo ili kuinusuru isiendelee kuharibiwa na mvua?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo - Lumecha (kilometa 284.5), sehemu ya Ifakara – Lupiro – Mtimbira (kilometa 112) kwa utaratibu wa sanifu na jenga (design and build). Ujenzi wa barabara hii utaenda pamoja na ujenzi wa mitaro kulingana na usanifu ulivyoelekeza. Kwa sehemu iliyobaki ya barabara hii, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itaendelea kuijenga mitaro kwa sehemu zenye uhitaji ili kuilinda barabara isiharibiwe na maji ya mvua, ahsante.