Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isijenge mitaro katika Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Namtumbo ili kuinusuru isiendelee kuharibiwa na mvua?
Supplementary Question 1
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi, kwanza niipongeze Serikali kwa majibu mazuri ambayo yanakusudia kwenda kuijenga barabara hii ambayo inaunganisha takrabani wilaya na mikoa miwili tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili, swali la kwanza, wakati huu ambapo mkandarasi ameingia mkataba kwa ajili ya kuijenga, barabara hii imeharibika kwa kipindi hiki cha mvua, ni yapi maelekezo ya Serikali kuhakikisha barabara hii inaweza kupitika kwa kipindi hiki wakati wananchi wanaendelea kusubiri utekelezaji na ujenzi wa kiwango cha lami? Ndivyo ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameniagiza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kwa ajili ya wananchi wa Makete, Mheshimiwa Waziri unaijua Barabara ya Makete Mbeya ni barabara ambayo mvua inanyesha kwa muda mrefu na wewe umekuwa ukikiri hapa mara kwa mara kwamba barabara hii inasumbua kwenye ujenzi wake. Ninavyozungumza sasa hivi mvua imesimama, hainyeshi tena, kiangazi kimeanza, lakini mkandarasi hajarekebisha barabara hii ili wananchi wangu waweze kupita katika mazingira salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba maelekezo ya Serikali muda huu, dakika hii, kwa mkandarasi yule ili barabara iweze kupitika na wananchi waendelee kufanya shughuli za kiuchumi kwenye Jimbo la Makete, ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Barabara ya Ifakara – Lupilo – Malinyi hadi Lumecha ilipata changamoto kubwa ya kuharibika na kimsingi ilikuwa haipitiki kabisa, lakini maeneo mengi ambayo yalikuwa hayapitiki ni yale yenye mito na sasa hivi nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kuna mto unaitwa Namhanga ambao ulikuwa umekata kabisa mawasiliano kati ya Malinyi na upande mwingine, tuna mipango miwili pale na hasa kwa wananchi wa Malinyi tuna mipango mitatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza ilikuwa ni kupeleka daraja la muda la chuma ambalo tayari tumeshaliweka na magari yenye uzito usiozidi tani kumi yanaendelea kupita, lakini mpango wa muda wa kati ni kujenga drift ili tuweze kuruhusu sasa magari yote yaweze kupita, lakini mpango wa kudumu ni kwamba tunaanza kujenga lile daraja kwa sababu lipo kwenye mpango wa kulijenga daraja lote ambalo tutasaidiana na wenzetu wa World Bank kupitia CRW hizo hela na tayari mkandarasi tumeshampata, kwa hiyo, tutahakikisha kwamba hiyo changamoto inaisha wakati huo mkandarasi atakayeanza kujenga kipande hicho cha kilometa 112 akiwa anafanya mobilization.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara hii ya Makete – Mbeya, nimwagize tu Meneja wa Mkoa wa Njombe ahakikishe kwamba wakandarasi hawa wanarudi site, lakini kabla ya kurudi site warekebishe maeneo yote ambayo yalikuwa yamekatika ndipo aanze kufanya kazi sasa ya ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isijenge mitaro katika Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Namtumbo ili kuinusuru isiendelee kuharibiwa na mvua?
Supplementary Question 2
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Daraja la Mangara limesimama ujenzi wake sasa hivi ni takribani kama miaka miwili hivi na sababu ni kwamba mkandarasi hajalipwa certificate zake, nimekuja mara kadhaa kwenye Wizara ya Ujenzi kwa ajili ya ku-push jambo hili na hata Mheshimiwa Naibu Waziri analifahamu vizuri, je, anataka kuzungumzia nini kuhusiana na daraja hili, sehemu ambapo takribani shilingi bilioni tano zimeingia, je, zinapotea bure tu?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hizo fedha haziwezi kupotea na Serikali itahakikisha kwamba inalikamilisha hilo daraja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, si kwamba tu hilo daraja ni muhimu kwa ajili ya wananchi na wanaolima korosho lakini pia ni daraja muhimu sana kwa shughuli za ulinzi kwa sababu ndiyo barabara ambayo tunasema barabara ya ulinzi kwa mikoa ya Mtwara na Ruvuma. Kwa hiyo tutahakikisha Mheshimiwa Mbunge baada ya mvua kukatika wakandarasi hao watarudi site ili kulikamilisha hilo daraja, ahsante.
Name
Halima James Mdee
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isijenge mitaro katika Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Namtumbo ili kuinusuru isiendelee kuharibiwa na mvua?
Supplementary Question 3
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Bunge lilielekeza Mfuko wa Barabara kukusanya kutokana na tozo ya mafuta shilingi bilioni 850, mpaka mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa shilingi bilioni 819; mpaka sasa hivi TANROADS wamepewa shilingi milioni 123 tu; lakini vilevile mnadaiwa na wakandarasi shilingi trilioni 1.3. Sasa kwa nini unawapa Wabunge majibu ambayo unajua hayatekelezeki kwa sababu hamna pesa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni kwamba nimuombe ili apate maelezo ya kina, nitamuomba afanye mambo mawili, ama atuletee swali lake la msingi ambalo litalingana na swali na tumpe maelezo sahihi, ama tuweze kuonana baada ya hapa maana swali la msingi hapa ni kujenga mitaro kwenye barabara kwa hiyo hili swali nadhani tumuombe atuletee swali la msingi tumjibu vizuri, ahsante. (Makofi)
Name
Shamsia Aziz Mtamba
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Mtwara Vijijini
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isijenge mitaro katika Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Namtumbo ili kuinusuru isiendelee kuharibiwa na mvua?
Supplementary Question 4
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili nami niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.
Ni lini Serikali itafanya ukarabati mkubwa Barabara yetu ya Kusini ya Somanga – Kibiti - Lindi kutokana na uharibifu mkubwa uliopo hivi sasa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, barabara hii ni barabara kuu ambayo inaenda Mikoa ya Kusini, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sasa ukienda kazi iliyokuwa inafanyika ni kujenga maeneo yote yaliyokuwa yameharibika na hasa ya madaraja, na tunachowekea sasa hivi ukienda utaona tayari tunasema tumeshakamilisha kazi ya chini na vyuma vimeanza kusimama. Maeneo yote yaliyokuwa yamechoka sasa hivi madaraja yale yanajengwa, lakini tuna mpango wa kuhakikisha kwamba tunakarabati maeneo yote yaliyokuwa yameharibika ambayo yalikuwa hayapitiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mpango upo na tumekuwa tunayaongezea mara kwa mara wakati tunatafuta fedha, chanzo kikubwa na ambacho kitakuwa cha uhakika kuikarabati barabara yote ya kusini, ahsante.