Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 558 2025-06-10

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question


MHE. NEEMA G. MWANDABILA K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Sepuka - Ndago hadi Kizaga?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Barabara ya Sepuka – Ndago ni sehemu ya Barabara ya Sepuka - Ndago - Kizaga yenye urefu wa kilometa 77.4. Serikali tayari imeanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Sepuka – Ndago – Kizaga kilometa 77.4 na hadi tarehe 30 Mei, 2025 kazi za ujenzi zilikuwa zimefikia asilimia tatu, ahsante. (Makofi)