Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Sepuka - Ndago hadi Kizaga?
Supplementary Question 1
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa barabara hii ni muhimu sana, wanawathibitishia vipi wananchi hawa kwamba barabara hii itaisha haraka?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, nilitaka kufahamu Barabara ya Mbalizi – Songwe – Mkwajuni, inaanza lini rasmi? Maana mlituambia mtatenga bajeti, hatujaona kinachoendelea site? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, barabara hii itaisha haraka kwa sababu tayari wakandarasi wako site na wameshalipwa advance na ndiyo maana wako wameanza kufanya kazi. Kwa hiyo, cha msingi tutawasimamia ili waweze kukamilisha kwa mujibu wa mkataba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mbalizi – Songwe, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tuko tayari muda wowote kusaini hii barabara kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami kama tulivyoahidi na bado tumeipangia tena kwenye bajeti ya mwaka unaokuja ili kuendelea na ujenzi, ahsante. (Makofi)
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Sepuka - Ndago hadi Kizaga?
Supplementary Question 2
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.
Ni lini Serikali itajenga Barabara ya Old Moshi kupitia Kikarara – Kidia mpaka Kirua ambayo ina kilometa 17 lakini Serikali imejenga kilometa 4.5 tu na barabara hii ni muhimu kwa sababu inaamua hatma ya uchumi wa kata zaidi ya tano. Ni lini Serikali itamaliza barabara hii? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli barabara hiyo ni muhimu na tutahakikisha kwamba tunashirikiana na wenzetu wa TARURA kuweza kuzijenga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge kwamba barabara zetu ni zile ambazo hasa zinaunganisha wilaya na wilaya, wilaya na mkoa na baadhi ambazo zinapita kwenye kata. Kwa hiyo, nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge Serikali tutahakikisha kwamba tunakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kwa hizo barabara alizozitaja, ahsante.

Supplementary Question 3

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Sepuka - Ndago hadi Kizaga?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ningependa kumuuliza Mheshimiwa Waziri, ni lini mkandarasi atarejea katika site ambapo alikuwa ameshaweka vifaa vyake lakini mwaka jana mwezi wa kumi akaviondoa na watu sasa wanasubiri barabara na mkandarasi hayupo? (Makofi)
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni barabara kutoka airport kwenda Kayenze ambayo inajengwa kwa kilometa 10 kutoka airport mpaka Kabangaja kwa awamu ya kwanza.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ningeomba anitajie hiyo barabara. Maana ninajua ana barabara mbili pale. Sasa sijajua ni ipi hasa.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayofanya kuhusu wananchi wa Ilemela. Nataka nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Mwanza, Serikali inachukulia barabara hii kama ni moja ya barabara ambayo ni bypass kwa watu wa kutoka airport wanaokwenda Mikoa ya Simiyu, Mara na Kenya. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mkandarasi huyu tumeshapokea hati zake za madai ya fedha za awali ili aweze kurudi site na kuanza kazi na akamilishe hizo kilometa 10, ahsante.
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Sepuka - Ndago hadi Kizaga?
Supplementary Question 5
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Wabunge kutoka Mikoa ya Tabora, Mbeya, Singida na Songwe, wangependa kusikia kauli ya Serikali kuhusu ukamilishaji wa barabara namba nane nchini (trunk road namba nane) ambayo kipande kutoka Ipole – Rungwa, Rungwa – Makongolosi na Rungwa – Itigi hadi Mkiwa, vitakamilika lini? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumjibu Mheshimiwa Kakunda na kwa niaba ya Wabunge aliowataja wa mikoa hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakiri kwamba hiyo barabara aliyoitaja sasa hivi ndiyo barabara iliyobaki, barabara ndefu na barabara kuu ya nchi ET8 na tulichopewa maelekezo ni kuhakikisha kwamba tunatafuta chanzo kikubwa cha fedha na tuko tayari tunaongea na taasisi mbalimbali za kifedha ambazo ziko tayari kuweza kuingia nazo ubia ili tuweze kujenga hiyo Barabara ya Ipole – Rungwa, lakini Mkiwa – Rungwa halafu Rungwa – Makongolosi. Kwa hiyo, tunajua itasaidia sana kuunganisha mikoa ya nyanda za juu Kusini, mikoa ya kati lakini na mikoa ya Kaskazini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali inaichukulia kwa umuhimu mkubwa sana hiyo barabara, ahsante. (Makofi)
Name
Ally Mohamed Kassinge
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kusini
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami Barabara ya Sepuka - Ndago hadi Kizaga?
Supplementary Question 6
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, barabara ya kutoka Masaninga – Nangurukuru mpaka Kilwa Masoko imeharibika vibaya sana kutokana na aidha mvua, lakini pia magari mazito yanayobeba uzito mkubwa ambayo yanapeleka materials kwenye ujenzi wa bandari kule Kilwa Masoko. Serikali iliahidi hapa kutenga fedha kwa ajili ya kuikarabati ama kuijenga upya barabara hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kutengeneza Barabara ya Masaninga – Nangurukuru – Kilwa Masoko?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kutokana na mabadiliko makubwa ya kiuchumi ni kweli kuna barabara ambazo zilikuwa zimejengwa kulingana na uzito ama aina ya magari yanayopita. Sasa hivi tulichofanya ni kuisanifu hiyo barabara kulingana na ukweli kwamba sasa inabeba ama inapitisha magari yenye uzito mkubwa ili sasa tuweze kuijenga kulingana na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, Serikali inalifahamu na tunalifanyia kazi, ahsante.