Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 560 2025-06-10

Name

Mustafa Mwinyikondo Rajab

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Primary Question

MHE. HAJI AMOUR HAJI K.n.y. MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka magari katika Vituo vya Polisi Wilaya ya Magharibi B?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi Mei, 2025 Serikali imepeleka gari jipya aina ya Toyota Land Cruiser Pickup kwa Wilaya ya Magharibi B Unguja na kufanya wilaya hiyo kuwa na magari mawili sasa. Serikali itaendelea kutenga fedha toka kwenye bajeti yake kila mwaka kwa ajili ya kununua magari na vitendea kazi vingine kwa matumizi ya Jeshi la Polisi na kugawa katika mikoa na wilaya zote hapa nchini, ahsante.