Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Haji Amour Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makunduchi
Primary Question
MHE. HAJI AMOUR HAJI K.n.y. MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka magari katika Vituo vya Polisi Wilaya ya Magharibi B?
Supplementary Question 1
MHE. HAJI AMOUR HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Kajibu vizuri lakini pia vilevile Wilaya ya Magharibi pamoja na kwamba kuna magari mawili ambayo yamepelekwa pale, lakini bado kuna vituo kama Kituo cha Kijitoupele ambacho kiko katika ndani ya Jimbo la Pangawe, kile kituo kina shida sana kwa sababu kina mkusanyiko wa mambo mengi mno.
Sasa sijui ni lini pamoja na kwamba kuna magari, lakini kwamba Serikali itaipelekea angalau zile pikipiki kwa kuweza kufanya patrol hasa kwa wakati ule wa kipindi cha uchaguzi? Ahsante. (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Haji Amour Haji, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Serikali ilishapeleka pikipiki zaidi ya 105 katika kata na shehia kwa upande wa Zanzibar na kwa sababu ametaja suala la uchaguzi, nikuhakikishie Serikali kupitia Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba maeneo yote yatakuwa salama, lakini pia tutaangalia namna ya kupekeka pikipiki katika eneo hilo ili kusaidia doria na kulinda usalama wa raia na mali zao katika eneo hilo, ahsante sana.
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAJI AMOUR HAJI K.n.y. MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka magari katika Vituo vya Polisi Wilaya ya Magharibi B?
Supplementary Question 2
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Kituo cha Polisi cha Tanangozi kina changamoto kubwa sana ya gari, lakini Waziri, Mheshimiwa Masauni aliahidi kupeleka samani pale katika kituo kile. Je, ni lini Serikali itapeleka samani na kuwapatia gari? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Grace Tendega, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali imeshasambaza magari kwa ajili ya ma-OCD wilaya zote hapa nchini na ifikapo mwezi Agosti tutakuwa tumesambaza pia magari kwa ma-OCD nchi nzima. Kwa hiyo, naamini magari yote haya mawili yakipatikana yatasaidia hapo katika eneo alilotaja Mheshimiwa Mbunge katika eneo lake la Tanangozi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu samani tumechukua pia kituo hicho tuingize kwenye mpango tayari kwa kutengewa fedha kwa ajili ya kuipatia samani ili ofisi iendelee kufanya kazi, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved