Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 15 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 182 | 2025-04-30 |
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara za lami katika Mji Mdogo wa Karatu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara za lami katika Mji wa Karatu ambapo hadi sasa jumla ya kilometa 3.595 zimejengwa kwa kiwango cha lami ambapo mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali ilijenga barabara yenye urefu wa kilometa 0.610 kwa gharama ya shilingi milioni 500. Aidha, mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali ilijenga barabara yenye urefu wa kilometa 0.725 kwa gharama ya shilingi milioni 475.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali vilevile, inaendelea kujenga barabara yenye urefu wa kilometa 0.710 kwa gharama ya shilingi milioni 469.5. Pia, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imeweka katika mipango yake kujenga barabara yenye urefu wa kilometa 0.9 kwa gharama ya shilingi milioni 604.2.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Mji wa Karatu na miji mingine nchini kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved