Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 15 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 183 2025-04-30

Name

Aleksia Asia Kamguna

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha lami?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakusudia kujenga kwa tabaka la lami barabara za Makao Makuu ya Wilaya zote hapa nchini ikiwemo Wilaya ya Malinyi. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali inaendelea na ujenzi wa Barabara ya Mnadani - Bomani inayoelekea Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa tabaka la lami yenye kilometa 0.85 kwa thamani ya shilingi milioni 759. mpaka sasa ujenzi bado unaendelea na umefikia 30%.