Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aleksia Asia Kamguna

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa nafasi na ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na jitihada ambazo inachukua katika Wilaya yetu, lakini katika Mkoa wa Morogoro miundombinu mingi imeharibika hususani katika Wilaya ya Malinyi na Wilaya ya Malinyi. Sasa hivi ninavyoongea mawasiliano ya barabara hakuna ukitoka mjini kwenda halmashauri ya mji ambapo ndipo kunapatikana huduma za jamii. Sasa hivi tunapita barabara ya mchepuko ambayo inaitwa Barabara ya Mchangani na hiyo barabara ni mbovu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; je, Serikali ipo tayari kutengeneza hiyo barabara kwa dharura ili wale watu wapite na pia itengenezwe kwa kiwango cha lami kupunguza adha wanazozipata hawa wananchi wanawake na watoto?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; katika Mkoa wa Morogoro Serikali inajitahidi sana kupeleka pesa ili kutengeneza hizo Barabara, lakini baada ya muda mfupi zile barabara zinaharibika. Je, Serikali inawachukulia hatua gani wakandarasi ambao wanatengeneza barabara hizo chini ya kiwango?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba swali la kwanza la Mheshimiwa Aleksia Kamguna kwamba barabara hii anayoizungumzia Barabara ya Mchangani ambayo kwa jina inaitwa Barabara ya Malinyi – Igawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli barabara hii ni barabara mbadala ya kuingia katika Mji wa Malinyi na usiku wa tarehe 16 Aprili, 2025, yalitokea mafuriko ambayo yanatokana na mvua za masika ambazo zinaendelea kunyesha Malinyi na barabara hii kimsingi mawsiliano yamekatika na mpaka wakati huu TARURA inachukua hatua za kidharura ili kuhakikisha kwamba inarudisha mawasiliano kwenye barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inafanya mpango wa kudumu wa kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami ili iweze kuwa katika mazingira mazuri na iweze kuhudumia wananchi katika kipindi cha mwaka mzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake la pili ni kwamba, Serikali inapotoa nafasi ya ujenzi wa barabara hizi kwa wakandarasi inatarajia kwamba wakandarasi waweze kuzingatia mkataba wanapokuwa wanatekeleza ujenzi wa barabara hizi za wilaya na Serikali inakuwa makini kusimamia viwango kwamba mikataba siyo tu inakwisha kwa wakati, lakini ujenzi pia uzingatie viwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuchukua hatua kwa wale wakandarasi ambao kwanza hawatimizi mikataba yao kwa wakati, lakini pia hawatimizi viwango ambavyo vinakusudiwa kimkataba katika ujenzi wa barabara hizi muhimu. Kwa hiyo, Serikali itaendelea kuchukua hatua hizo kuhakikisha kwamba barabara zetu zinajengwa kwa viwango na zinaweza kudumu kwa muda mrefu baada ya kuwa zimejengwa.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2


MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya Bujela, Masukulu, Matwebe ni barabara ya kimkakati na ni nzuri sana tuliiombea wakasema wataiwekea kiwango cha lami ni lini wataitekeleza ahadi hiyo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inafanya uwekezaji mkubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara na hasa barabara zetu hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA na utaiona dhamira ya Serikali hata kwenye upande wa kutenga bajeti kwa ajili ya barabara hizi za TARURA wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani bajeti ya TARURA ilikuwa ni bilioni 275, lakini mpaka wakati huu tunapozungumza bajeti hiyo imeendelea kuongezeka kila mwaka na tunatarajia mwaka wa fedha 2025/2026 bajeti ya TARURA itakuwa ni trilioni 1.18.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo tunaona kabisa dhamira ya kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara hizi muhimu za wilaya. Ninaomba niendelee kumuhakikishia Mheshimiwa Sophia Mwakagenda kwamba barabara hii aliyoitaja na miundombinu ya eneo hili alilolitaja Serikali itafika na itaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhakikisha inaimarisha miundombinu hii ili iweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi, lakini iwawezeshe kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii.

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya kwa Mtoro Sanzawa hadi Mpendwe yenye kilometa 54 iliharibiwa kabisa na mvua za 2023/2024 tulishaleta maombi ya fedha TARURA. Ninaomba kujua ni lini sasa Serikali itatoa fedha hizo ili tuweze kurekebisha barabara hii? Ahsante sana.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuendelea kumuhakikishia Mheshimiwa Mohamed Monni kwamba kwa kweli amekuwa akifanya ufuatiliaji wa karibu sana kuhakikisha miundombinu ya barabara katika jimbo lake inaweza kupatiwa fedha na inaweza kuimarishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie kwamba maombi tumeyapokea na tunayafayia kazi na fedha zitaletwa kwa ajili ya kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara hizi zinazosimamiwa na TARURA katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge.

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4


MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kujenga kwa kiwango cha lami kilometa tano pale Mji wa Usa River ambazo zilitolewa mwaka 2015 na Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Dkt. Pallangyo ambaye kwa kweli amekuwa akifanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha kwamba miundombinu ya barabara hizi za wilaya zinasimamiwa na TARURA zinaweza kujengwa na kuweza kuwanufaisha wananchi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie kwamba Serikali italeta fedha kuhakikisha kwamba barabara hizi ulizozitaja katika eneo la Usa River zinajengwa kwa kiwango cha lami ili ziweze kuwanufaisha wananchi wako. Kilio chako na sauti yako na sauti ya wananchi wako imesikika na Serikali sikivu Serikali ya Awamu ya Sita itahakikisha inaleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo muhimu kabisa katika jimbo lako.

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 5

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa sababu ya mvua zinazoendelea hali ni mbaya kwenye maeneo mengi sana na TARURA hawana fedha ya dharura kwa ajili ya kukabiliana na dharura hii ni nini kauli ya Serikali juu ya jambo hili? Ninakushukuru.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer


NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Timotheo Mnzava kwamba kila mwaka wa bajeti, Serikali inatenga fedha ya dharura. Pia, ninaomba nimpe taarifa njema kwamba katika mwaka huu wa bajeti, Bunge hili Tukufu limepitisha nyongeza ya bajeti ya shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kutengeneza barabara ambazo zimeharibika kutokana na madhara mbalimbali ikiwemo madhara ya mvua kwa dharura.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itachukua hatua ya dharura kuhakikisha kwamba inarudisha mawasiliano kwenye maeneo ambayo mawasiliano yamekatika na kuimarisha miundombinu ya barabara hizi za wilaya ili ziweze kupitika katika kipindi cha mwaka mzima na ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi pamoja na kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii. Kwa hiyo, ninaomba Mheshimiwa Mbunge afahamu kwamba tutafika katika Jimbo lake kuhudumia maeneo ambayo mawasiliano yamekatika na tutachukua hatua za kidharura.