Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 15 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 184 2025-04-30

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kutoa mshahara kwa Madiwani ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Waheshimiwa Madiwani katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo na huduma za jamii katika mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa, Waheshimiwa Madiwani hulipwa posho za kila mwezi kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Halmashauri na Waraka wa Serikali wa Desemba, 2014 na Waraka wa Aprili, 2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia kwamba nafasi ya udiwani ni ya muda maalum wa uongozi na sio ajira ya kudumu inayohusisha utumishi wa moja kwa moja ndani ya mfumo wa Serikali, malipo ya posho yameendelea kuwa njia nzuri ya kutambua mchango wa Waheshimiwa Madiwani, ahsante.