Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutoa mshahara kwa Madiwani ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; je, Serikali haioni kukosekana kwa mishahara na posho isiyoridhisha kwa Madiwani ni chanzo cha rushwa na kuzoroteshwa kwa miradi katika maeneo yanayosimamiwa na Madiwani?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa maeneo ya usimamizi ya kiutawala ya Madiwani ni makubwa kuliko posho wanayopata; je, Serikali haioni ipo haja ya kuwapatia Madiwani usafiri kama vile ambavyo CCM imeweza kufanya kwenye kata zake? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hii inatambua, mchango mkubwa sana wa Waheshimiwa Madiwani katika kusimamia halmashauri zetu, kusimamia miradi ya maendeleo na huduma za kijamii kwa ujumla. Pia, Serikali hii inathamini sana mchango wa Waheshimiwa Madiwani na ndiyo maana Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali Kuu ilichukua jukumu la kulipa posho za Waheshimiwa Madiwani kwa 95% ya halmashauri zetu kote nchini ili kuwawezesha kwanza kuwa na uhakika kwa kupata posho zao kwa wakati, lakini pili kupata posho hizo ambazo pia ziliongezwa kiwango.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunafahamu kwamba bado kiwango cha posho za Waheshimiwa Madiwani hakitoshelezi, lakini Serikali inaendelea kujiongezea uwezo wa ukusanyaji wa mapato ili kadri uwezo unavyoongezeka tuendelee kuongeza posho za Waheshimiwa Madiwani na waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, tunafahamu, ni kweli wapo Waheshimiwa Madiwani ambao wana kata kubwa sana na wana changamoto ya usafiri. Serikali itaendelea kufanya tathmini na kuona uwezekano wa kupata vyombo vya usafiri kwa kadri uchumi utakavyokuwa unaruhusu ili Waheshimiwa Madiwani waendelee kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi. Ahsante sana.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutoa mshahara kwa Madiwani ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu?

Supplementary Question 2

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakubaliana na majibu ya Serikali, lakini kwa kweli posho za Madiwani ni ndogo sana. Je, ni lini Serikali itafanya mapitio ili kuboresha kipato cha Madiwani? Ahsante.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekwishafanya tathmini na inatambua kwamba kweli posho za Waheshimiwa Madiwani hazitoshelezi. Hata hivyo, ili kuwa na kiwango kikubwa cha posho, lazima tujenge kwanza uwezo wa mapato ya Serikali yenyewe ili iweze kumudu kulipa posho hizo za Waheshimiwa Madiwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge kote nchini kwamba Serikali inatambua sana mchango wao katika usimamizi wa shughuli mbalimbali katika halmashauri na ndiyo maana imechukua jukumu la kulipa posho katika halmashauri zaidi ya 95% badala ya siku za nyuma ambapo halmashauri zilikuwa hazina uwezo wa kuwalipa hata hizo posho za kila mwezi na kuwezesha Waheshimiwa Madiwani kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kadri Serikali itakavyoendelea kujenga uchumi na uwezo wake wa mapato ya ndani, tutaendelea kuona uwezekano wa kuongeza posho za Waheshimiwa Madiwani. Ahsante sana.