Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Finance and Planning Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 185 2025-04-30

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka Watumishi wa Afya wa kutosha wa Kike - Ukerewe ili kulinda haki ya kijinsia ya Mtoto wa Kike?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya watumishi wa Afya 381. Kati ya hao watumishi 197 ni watumishi wa kike na watumishi 184 ni watumishi wa kiume.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ajira ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, Halmashauri ya Ukerewe imepokea watumishi 30 ambapo watumishi 18 ni wa kike na watumishi 12 ni wa kiume. Serikali imekuwa ikizingatia uwiano wa kijinsia wakati wa kuajiri watumishi wa afya na kuwapanga katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.