Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Watumishi wa Afya wa kutosha wa Kike - Ukerewe ili kulinda haki ya kijinsia ya Mtoto wa Kike?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Ninatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali na nitumie nafasi hii kuwapongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kwenye maeneo ya pembezoni, kwa mfano tuchukulie Zahanati ya Kulazu, Kisiwa kidogo cha Ilugwa haina mtumishi wa kike, Zahanati ya Kwelu kwenye Kisiwa kidogo cha Kwelu haina mtumishi wa kike na Zahanati ya Busumba kwenye Kisiwa kidogo cha Bwilo haina mtumishi wa kike. Jambo hili linaleta changamoto kubwa na sababu kubwa inayopelekea watumishi wa kike kukimbia maeneo haya ni kwa sababu ya mazingira magumu hasa kukosa nyumba za watumishi. Nini sasa mkakati wa Serikali kuweka mazingira mazuri hasa ujenzi wa nyumba za watumishi ili hao watumishi wa kike waweze kukaa na kuhudumia wananchi wetu? Ninashukuru sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaomba nianze kwa kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba katika Sekta ya Afya na katika utoaji wa huduma za afya, wataalam wa kike na wataalam wa kiume siyo kigezo cha kutoa huduma bora katika vituo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi yapo mazingira ambayo wateja au wagonjwa wa kike wangeweza kuhudumiwa zaidi na wauguzi wa kiume au madaktari wa kiume na kinyume chake. Kwa hiyo, kwanza, ninaomba niweke hii rekodi sahihi zaidi, kwamba hakuna utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila zahanati ina mtumishi wa kike na kama haina mtumishi wa kike kwamba zahanati hiyo haina watumishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu ni kwamba mtumishi yeyote awe wa kike au wa kiume amekuwa trained, ana miiko, ana utaalam na anaweza kutoa huduma za afya kwa muktadha huo. Kwa hiyo, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba eneo hilo la jinsia si eneo muhimu sana katika Sekta ya Afya, suala ni mtaalam anayeweza kutoa huduma hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na nyumba za watumishi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mkundi kwamba Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeanza ujenzi wa nyumba za watumishi na hasa katika vituo vya pembezoni zaidi ikiwemo Halmashauri ya Ukerewe. Juzi tulikuwa pale tumeona kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali itaendelea kujenga nyumba za watumishi katika vituo vya pembezoni ili watumishi waweze kufanya kazi katika mazingira bora zaidi. Ahsante.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Watumishi wa Afya wa kutosha wa Kike - Ukerewe ili kulinda haki ya kijinsia ya Mtoto wa Kike?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, Vituo vya Afya vya Kasekese, Sibwesa na Bulamata ni miongoni mwa vituo ambavyo havina watumishi wa kutosha katika hayo maeneo. Ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha kwenye maeneo hayo? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Halmashauri ya Tanganyika na katika hivyo vituo vya afya ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja vina upungufu wa watumishi. Hata hivyo, Serikali hii ya Awamu ya Sita na ni dhamira ya dhati kabisa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki cha miaka minne ya Serikali hii, jumla ya watumishi 32,750 wameajiriwa na kupelekwa katika vituo vya huduma za afya kote nchini. Katika halmashauri ya Tanganyika wamepata pia watumishi wa Sekta ya Afya na tunaendelea kuwapeleka watumishi hao kwa awamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua upungufu huo na kila kibali cha jira kikitokea tutahakikisha tunatoa kipaumbele katika Halmashauri ya Tanganyika na zile nyingine ambazo ziko mazingira ya pembezoni.