Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 43 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 186 | 2025-04-30 |
Name
Salim Mussa Omar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Gando
Primary Question
MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza:-
Je, ni lini ahadi ya Serikali ya kuzuia maji chumvi kuingia katika Bonde la Mpanja Gando itatekelezwa?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi zinazochangia kuongezeka kwa kina cha Bahari kunakosababisha maji ya chumvi kuingia katika Bonde la Mpanja, Gando. Hatua hizo ni pamoja na kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia kurejesha maeneo yalioathirika kwa kuandaa maandiko ya miradi na kuwasilishwa kwa wadau wa maendeleo ikiwemo Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund) na Benki ya Dunia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muktadha huo, shughuli za kuzuia maji chumvi katika Bonde la Mpanja Gando zitaanza kutekelezwa baada ya fedha kupatikana kupitia miradi hiyo ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuendelea na shughuli zao. Ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved