Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Salim Mussa Omar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Gando
Primary Question
MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza:- Je, ni lini ahadi ya Serikali ya kuzuia maji chumvi kuingia katika Bonde la Mpanja Gando itatekelezwa?
Supplementary Question 1
MHE. SALIM MUSSA OMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na ninashukuru kwa majibu mazuri na yenye kutia matumaini ya Serikali, lakini nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza ambayo ningependa kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa kilimo kile ni kilimo cha matumizi ya chakula moja kwa moja kwa wananchi wa Jimbo la Gando na wewe mwenyewe pamoja na Mheshimiwa Kijaji (Waziri yule aliyepita) walikuja wakajionea mashamba haya takribani 200 yameendelea kuathirika siku hadi siku. Je, katika maandiko hayo ambayo wameandaa, wako tayari kuweza kuipa priority maalum Shehia hii ya Jimbo la Gando ili kusudi kuweza kuwalinda na janga la njaa wananchi hawa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa tatizo hili halipo Gando tu kwa Zanzibar, limekuwa ni tatizo kubwa na linaendelea kutuathiri sana; je, ni mpango upi mahususi wa Serikali walioupanga kwa ajili ya kuweka constant budget kuweza ku-overcome challenge hii?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana. Ninaomba nimjibu maswali mawili ya nyongeza lakini nichukue fursa hii kumpongeza sana kwa kuliona hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumefika katika Kijiji cha Mpanja katika Jimbo la Gando mimi na Mheshimiwa Kijaji wakati ule na tuliona athari kubwa ambayo wananchi wanaathirika. Maji ya bahari yameingia kwenye vipando ambavyo havistahimili maji ya bahari lakini pia maji ya bahari yameingia kwenye makazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tayari tumeshaomba dola za kimarekani milioni 10, tumeshaziomba na katika hizo tayari milioni 3.5 zinakuja kushughulikia tatizo kwa upande wa Zanzibar. Nimwambie Mheshimiwa aendelee kuwa na subira, tupo tunafanya utaratibu, zitakapopatikana tutahakikisha Gando na maeneo mengine yakiwemo Nungwi na maeneo mengine ya Lindi na Mtwara tunakwenda kuondoa hii changamoto.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba, pia tutahakikisha Jimbo la Gando tunalipa priority kwa sababu ya umuhimu na changamoto ambayo tumeiona imejitokeza pale.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved