Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 187 2025-04-30

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:-

Je, lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Kata za Jimbo la Mbagala ikiwemo Chamazi, Mianzini, Kilungule, Charambe, Mbagala, Kiburungwa na Kijichi Mbagala Kuu Maji litaisha?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Jimbo la Mbagala katika maeneo tajwa kunatokana na kuzidiwa kwa Kituo cha Kupoza Umeme cha Mbagala. Ili kutatua changamoto hii, Serikali kupitia TANESCO imefunga transfoma yenye uwezo wa MVA 120 katika kituo hicho na inatarajia kuiwasha hivi karibuni. Aidha, Serikali inatarajia kufunga nyaya zenye uwezo mkubwa katika njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 132 kutoka Kinyerezi hadi Mbagala kupitia Gongolamboto.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwingine, TANESCO inaendelea na usimamizi wa Mradi wa kuipatia Wilaya ya Mkuranga kituo kikubwa cha kupozea umeme chenye uwezo wa MVA 240 eneo la Dundani na kuacha utegemezi kwenye Kituo cha Mbagala. Kukamilika kwa miradi hii kutasaidia kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Jimbo la Mbagala. Ahsante.