Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Kata za Jimbo la Mbagala ikiwemo Chamazi, Mianzini, Kilungule, Charambe, Mbagala, Kiburungwa na Kijichi Mbagala Kuu Maji litaisha?

Supplementary Question 1

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kutokana na Jimbo la Mbagala kuwa na wananchi wengi na wanaongezeka siku hadi siku; je, Serikali haioni ipo haja ya kujenga substation nyingine katika eneo la Chamazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kutokana na ubadilishaji wa nguzo unaoendelea hivi sasa, kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme zaidi ya saa 18 kwa siku. Je, Serikali haioni ipo haja ya kupunguza mgao huu na kufanya saa zikawa nane?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru na nimpongeze sana Mheshimiwa Chaurembo, kwa kweli amekuwa akifuatilia kwa muda mrefu jambo la kuimarika kwa hali ya umeme katika Jimbo la Mbagala.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kujenga substation (kituo cha kupooza umeme) katika eneo la Chamazi. Ni kweli Kituo cha Kupooza umeme Mbagala kinahudumia maeneo mengi sana; Mbagala, Yombo, Chamazi mpaka Mkuranga. Tulipofanya tathmini, eneo la Mkuranga lina load kubwa sana na ndiyo maana kipaumbele kikawepo kwamba kupitia mradi wetu wa North East Grid tujenge kwanza kituo cha kupooza umeme pale Mkuranga chenye uwezo wa MVA 40 kwa ajili ya kupunguza laod kubwa ambayo ipo katika Kituo cha Kupooza Umeme cha Mbagala.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mradi huu utakapokamilika, Kituo cha Kupooza Umeme cha Mbagala kitakuwa kimeondolewa na load kubwa sana na hivyo kuimarika kwa hali ya umeme katika Jimbo la Mbagala. Pia, huko mbeleni tutaendelea kutafuta bajeti kwa ajili ya kuendelea kujenga vituo vya kupooza umeme kulingana na mahitaji yatakayokuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na hali ya kukatika kwa umeme. Ni kweli tulikuwa tunafanya maboresho katika line ambazo zinahudumia baadhi ya maeneo hususan katika eneo la Mbande. Kwa hiyo, makubaliano ilikuwa ni kwamba tunapofanya marekebisho umeme ukosekana kwa saa nane tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, nimwelekeze Meneja wa Mkoa na Meneja wa Wilaya wahakikishe makubaliano tuliyokubaliana nao ya saa nane tunapofanya matengenezo, hayo ndiyo yabaki. (Makofi)

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Kata za Jimbo la Mbagala ikiwemo Chamazi, Mianzini, Kilungule, Charambe, Mbagala, Kiburungwa na Kijichi Mbagala Kuu Maji litaisha?

Supplementary Question 2

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mkoa wa Rukwa bado tunatumia umeme kutoka Zambia na umeme unakatika sana na kuleta kero kwa wananchi. Wizara ina mkakati gani wa haraka wa kuondoa kero hiyo kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa ya umeme kukatika mara kwa mara?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, jana wakati tunahitimisha bajeti nilielezea kuhusiana na mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme wa Gridi katika Mkoa wa Rukwa. Kwa sasa tunao Mradi unaitwa TAZA ambao unajenga line kutokea Iringa, Tunduma hadi Rukwa kwa ajili ya kufikisha umeme wa Gridi katika Mkoa wa Rukwa. Ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Mkoa wa Rukwa, Serikali iko kazini. Mkandarasi ni mzuri sana na yupo site kuhakikisha anajenga line ya umeme na vituo vya kupooza umeme ili mwisho wa siku tuweze kufikisha umeme wa Gridi Mkoani Rukwa kama ambavyo Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi alipofanya ziara Mkoa wa Rukwa na Mheshimiwa Rais alifanya ziara pia na aliahidi jambo hilohilo. Mkandarasi yupo site, kazi inaendelea.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Kata za Jimbo la Mbagala ikiwemo Chamazi, Mianzini, Kilungule, Charambe, Mbagala, Kiburungwa na Kijichi Mbagala Kuu Maji litaisha?

Supplementary Question 3

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa tatizo la kukatikatika kwa umeme limekuwa sugu sana katika Jimbo la Vwawa, Wilaya ya Mbozi na Mkoa wa Songwe; je, zipi hatua za dharura za kuhakikisha kwamba tunanusuru tatizo hilo?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Songwe yanapewa umeme kupitia substation ambayo iko Mbeya. Kwa hiyo, kupitia Mradi huu wa kupeleka Gridi Mkoa wa Rukwa, Kituo cha Kupooza Umeme kitajengwa pale Songwe na hivyo kusababisha baadhi ya majimbo pale likiwemo Jimbo la Mheshimiwa Mbunge wasiweze kupata umeme kwa kutumia line kubwa ambayo ni ndefu sana jambo linalosababisha kukatikatika kwa umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkandarasi yuko site, kazi imeanza na mradi ukikamilika, wananchi wa jimbo lako wataona mabadiliko hayo kwa sababu tunajenga kituo cha kupooza umeme pale kwa ajili ya kuzuia line ndefu wawe wanapata umeme kwa kutokea karibu ili uendelee kuimarika. Ahsante.

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza:- Je, lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Kata za Jimbo la Mbagala ikiwemo Chamazi, Mianzini, Kilungule, Charambe, Mbagala, Kiburungwa na Kijichi Mbagala Kuu Maji litaisha?

Supplementary Question 4

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kumekuwa na shida ya kukatika umeme usiku mara kwa mara katika njia kuu ambayo inatoka Kata ya Luwegu, Luchili, Mkongo, Limamu, Nalisimonji, Ligela, Lusewa hadi Magazini; je, Serikali inaweza kuielekeza TANESCO waangalie shida ni nini kila inapofika usiku umeme huwa unakatika? Ahsante sana.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa swali la Mheshimiwa Mbunge na tutalifanyia kazi kwa umahususi. Kwa niaba ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu, ninaomba nimwelekeze Meneja wa Mkoa wa Ruvuma afanye jambo hilo kwa haraka. Wafanye survey kugundua tatizo ni nini, baada ya hapo tutafanya marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Wilaya ya Namtumbo, Serikali inao mkakati wa kujenga kituo cha kupooza umeme pale katika awamu ya pili ya Mradi wa Gridi Imara. Hata hivyo, kwa sababu Namtumbo ni Wilaya ya kimkakati kuna madini muhimu sana, tunaona uwezekano wa kuharakisha zoezi hilo kwa ajili ya kuimarisha hali ya umeme Namtumbo kwa ajili ya shughuli hii ya kiuchumi ya madini muhimu ambayo yapo pale.