Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 15 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 190 2025-04-30

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mnamo tarehe 13 Novemba, 2015 Serikali kupitia UCSAF iliingia makubaliano na kampuni ya Honora (Yas) kujenga mnara katika Kata ya Mkalamo. Pia, mnamo tarehe 13 Desemba 2018 UCSAF iliingia makubaliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili kufikisha mawasiliano katika Kata hiyo ambapo ujenzi wa minara yote miwili ilikamilika kwa kujengwa katika Vijiji vya Magamba na Mpasilasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kutokana na changamoto kubwa katika Kata ya Mkalamo mtoa huduma Honora alijenga minara mingine miwili katika vijiji vya Kwaisewa na Toronto Mbugani na kuifanya Kata hii kuwa na idadi ya minara minne.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ameuliza swali kuhusu Serikali kupeleka mawasiliano katika Kata husika, inaashiria kuwa bado kuna changamoto. Hivyo, Wizara kupitia UCSAF itafanya tathmini katika kata hiyo ili kubaini mahitaji halisi ya mawasiliano na endapo itabaini kuwepo kwa tatizo la mawasiliano katika kata hiyo ambapo itaingizwa katika zabuni ya miradi itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Kata za Magila, Gerezani na Kalalani, Serikali kupitia UCSAF itazifanyia tathmini Kata hizi ili kubaini changamoto za mawasiliano zilizopo na zitajumuishwa katika zabuni zitakazotangazwa katika mwaka wa fedha 2025/2026.