Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Timotheo Paul Mnzava
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Vijijini
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 1
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali tuna changamoto kubwa sana ya mawasiliano kwenye baadhi ya vijiji vya Kata ya Mkalamo eneo la Magila, Gereza kwa maana ya kwa Sunga ambayo ni Makao Makuu ya Halmashauri na eneo la Kigwasi mahali ambako kuna mgodi wa madini. Ninataka kujua hii tathmini ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri anasema wataifanya itafanyika lini?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Jimbo la Korogwe vijijini tulikuwa na ahadi ya kujengewa minara na bado kuna minara mitatu mpaka sasa hivi bado haijajengwa. Ninataka kujua ni nini kauli ya Serikali juu ya ujenzi wa hii minara mitatu ambayo haijajengwa? Ninashukuru.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, tathimini itafanyika lini Mheshimiwa Mbunge Mnzava amefuatilia sana hili, ninamwomba tuendelee kuwasiliana namna ambavyo amekuwa akifanya, lakini tutahakikisha ndani ya mwaka ujao wa fedha haya maeneo yote mawasiliano yanakwenda kuimarika na tathmini itafanyika kwa haraka sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika hii minara mitatu ambayo bado haijajengwa pia niendelee kumpongeza kwa namna ya ufuatiliaji wake wa karibu, nimeshaongea na wataalam wetu wanaendelea kufuatilia kuona minara hii iweze kujengwa mapema iwezekanavyo kadri fedha tunavyopata ndani ya mwaka huu wa fedha, lakini pia kufika mwaka ujao wa fedha tutahakikisha minara hii inakamilika.
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 2
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Je, ni lini mnara wa kutoka Kijiji cha Msasa Kata ya Busanda utakamilika?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Magessa, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kijiji hiki cha Msasa mnara huu tunautarajia ukamilike ndani ya mwaka huu wa fedha na Mheshimiwa Waziri Jerry Silaa ameshaagiza minara hii yote ambayo imeanza ujenzi lazima ikamilike ndani ya muda. (Makofi)
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Mashariki
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Vijiji vya Simbanguru na Kapiti Manyoni havina mawasiliano ya simu. Ni upi mkakati wa Serikali wa kupeleka mawasiliano ya simu katika vijiji hivyo? Ahsante sana.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Chaya, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika vijiji hivyo alivyovitaja Wilayani Manyoni Serikali dhamira yake ni kuhakikisha maeneo yote vijijini yanapata mawasiliano ya uhakika, kama vijiji hivi havipo kwenye 758, havipo kwenye 632 nimtoe shaka katika minara ambayo itapewa TTCL pamoja na watoa huduma wengine tutahakikisha tunakwenda kujenga katika mwaka ujao wa fedha.
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, niliuliza swali hapa kuhusiana na mawasiliano kwamba Serikali inazidi kuboresha mawasiliano na kila siku tunaongeza mawasiliano maeneo yasiyofikika, lakini pamoja na maendeleo hayo mazuri utapeli pia umezidi kuendelea kutapeli watu.
Mheshimiwa Naibu Spika, jina langu limekuwa likitumika mara kwa mara na leo ni mara ya tatu ninazungumza hapa. Nini kauli ya Serikali katika kusafisha majina ya watu ambayo yanazidi kuchafuliwa kwa maendeleo ya mtandao lakini bado watu wanaibiwa kwa kutumia majina ya viongozi. Ahsante. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Angeline Mabula, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, utapeli umeendelea, lakini watu wetu wa TCRA wameendelea na kazi nzuri sana ya kuhakikisha matapeli wote wanafahamika na wanakomeshwa. Hili tunaendelea kujipanga kwa hatua ngumu zaidi kuona kwamba tunaenda kukomesha kabisa suala la utapeli na suala la Mheshimiwa Angeline Mabula nimeshalifikisha kwa DG - TCRA Dkt. Bakari. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge nitaendelea kuwasiliana na Dkt. Bakari kuona kwamba hili suala linakomeshwa kabisa.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 5
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kata ya Bukundi kuna maeneo ambayo mawasiliano ya simu hayapo kabisa. Pia kuna Mwagotolo, Mwashimba, Mwashigela, Kasela na Mwanjolo. Je, ni lini Serikali itaimarisha mawasiliano?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, kata hii aliyoitaja Mheshimiwa Minza kama ni tatizo ni suala la umeme, watoa huduma wetu wamekuwa wakitumia source ya umeme kama solar, lakini maeneo mengine ambayo tayari TANESCO wamefanya kazi nzuri tunaendelea kuwahimiza watoa huduma wahakikishe wanapeleka umeme wa REA kwenye minara hii, hivyo maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Minza na yenyewe tutaendelea kuyafuatilia na kuyasimamia kuhakikisha mawasiliano yanakuwa ya uhakika.
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 6
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Lwande kuna mnara wa Halotel, lakini kwa kweli kiuhalisia mawasiliano hakuna. Sasa ninaomba nimuulize Naibu Waziri ni nini mpango mkakati kuhakikisha kwamba Kata hii ya Lwande mawasiliano hasa ya Halotel yanapatikana muda wote? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kigua kuhusu Kata ya Lwande mnara wa Halotel upo, lakini haufanyi vizuri, Mheshimiwa ninamhakikishia kwamba nitaufuatilia kuona tatizo ni nini, kama ni suala la umeme basi tutaendelea kuwashauri watoa huduma hawa kuimarisha mnara huu ili lengo la kusababisha mawasiliano ya uhakika liweze kutimia.
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka mawasiliano ya simu kwenye Kata za Mkalamo, Magila, Gereza na Kalalani – Korogwe Vijijini?
Supplementary Question 7
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Kata ya Ovada, Kata ya Lalta Wilaya ya Chemba ina changamoto kubwa sana ya mawasiliano pamoja na uwepo wa minara ya TTCL, lakini wananchi hawa mawasiliano yao yamekuwa ni ya taabu ambayo hayana uhakika. Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kuboresha mawasiliano katika hizo Kata mbili?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILINAO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata hizi mbili alizozitaja katika Wilaya ya Chemba, TTCL tayari wamejenga mnara tutakachohakikisha kukisimamia kama Wizara ni kuona kwanza waweze kufanya huduma ya mashirikiano kwa pamoja ili hata watoa huduma wengine waweze kutumia mnara huu kusambaza huduma ya mawasiliano, TTCL pia kuhakikisha mnara huu wana u-upgrade wanauwekea uwezo wa kuona kwamba mawasiliano yaliyokusudiwa yanaweza kuwafikia wananchi.