Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 15 Water and Irrigation Wizara ya Maji 191 2025-04-30

Name

Seif Khamis Said Gulamali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manonga

Primary Question


MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:-

Je, lini Serikali itatenga fedha ili wananchi wa Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale – Manonga wapate maji ya Ziwa Victoria?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika baadhi ya Kata zilizopo Jimbo la Manonga Wilaya ya Igunga ikiwemo Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale. Katika kutatua changamoto kwenye Kata hizo, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi miwili mikubwa ya Ziba - Nkinga awamu ya pili pamoja na Nkinga - Simbo ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kukamilika kwa miradi hiyo kutanufaisha zaidi ya wakazi 70,000 waishio kwenye vijiji 17 vya Jimbo la Manonga, Wilaya ya Igunga.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali vilevile inaendelea na uchimbaji wa visima vitano katika Jimbo la Manonga unaoambatana na ujenzi wa miundombinu rahisi ya kutolea huduma (point source) katika baadhi ya vijiji vya Kata za Igoweko na Tambalale kupitia programu maalum ya uchimbaji wa visima 900.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha huduma ya maji kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo kadri fedha zinavyopatikana. Ninakushukuru. (Makofi)