Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha ili wananchi wa Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale – Manonga wapate maji ya Ziwa Victoria?
Supplementary Question 1
MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo ya nyongeza. Ni kweli tumepata utanuzi wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria Ziba - Nkinga. Ni kweli tumepata mkandarasi wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria Nkinga – Nsimbo. Ni kweli tumepata gari la kuchimba visima vitano kila Jimbo nasi tukiwemo, hasa katika maeneo ya Kata alizozitaja.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika ule mradi wa visima vitano kwenye kila Jimbo tumepata gari kwenye Kata ya Igoweko, Kata ya Uswaya na Kata ya Tambalale, katika maeneo yote haya matatu tumekosa maji chini ya ardhi, ndiyo tunaiomba sasa Serikali kupitia Wizara ya Maji kwamba, mradi ule wa maji ya Ziwa Victoria unapofika Nsimbo tuwekewe fedha za maji kutoka Nsimbo kwenda kwenye hizo Kata ya Igoweko, Kata ya Uswaya na Kata ya Tambalale. Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa ninakushukuru wewe na nimshukuru Mheshimiwa Seif Khamis Said Gulamali Mbunge wa Manonga kwa ushirikiano mzuri anaotupatia sekta ya maji na vilevile kwa kutoa ushirikiano pale ambapo tunapata changamoto.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa tumechimba visima vitano na visima vitatu hatukupata maji lakini tukaongeza kingine vikafika vitatu, visima viwili vinatoa maji mpaka sasa, lakini kimoja tunaendelea na ujenzi wa miundombinu. Vilevile ombi lake na ushauri wake Serikali tunaendelea kupokea ushauri wa wadau nasi kwa sababu maji ya Ziwa Victoria ambayo Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Hassan Suluhu alitoa Bilioni 680, kutoka Ziwa Viktoria mpaka Nzega - Igunga na extension yake ya Sikonge - Urambo pamoja na Kaliua bilioni 143 haya maji ni mengi sana. Kwa hiyo, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaweka katika bajeti yetu ijayo ili tuweze kuhakikisha kwamba, tunafanya extension katika maeneo ambayo tumekosa maji chini ya ardhi kutokana na uchimbaji wa kisima. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha ili wananchi wa Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale – Manonga wapate maji ya Ziwa Victoria?
Supplementary Question 2
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Ujenzi wa Mradi wa Makonde unasuasua kwa sababu, kuna changamoto ambazo mkandarasi bado anazo. Je, Serikali ina mkakati gani wa haraka wa kutatua changamoto za mkandarasi huyo, ili ujenzi uendelee?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Ninatambua kwamba, Mradi huu wa Makonde ni mradi wa kimkakati kwa Kanda ya Kusini. Serikali imekaa chini na mkandarasi kujadiliana namna ya kuzimaliza changamoto hizi, ili mradi huu uendelee. Pia, tunatambua kwamba, alikuwa na madai yake na wenzetu Wizara ya Fedha, tumeshaongea, tuko katika hatua nzuri, ili mkandarasi huyu aweze kurudi site mradi huu ukimbie kwa haraka na wananchi wapate wanachokitarajia kutokana na Mradi huu wa Makonde. Ahsante sana.
Name
Shamsia Aziz Mtamba
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Mtwara Vijijini
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha ili wananchi wa Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale – Manonga wapate maji ya Ziwa Victoria?
Supplementary Question 3
MHE. SHAMSIA A. MATAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi, ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya maji ambayo ipo kwa muda mrefu katika Kata ya Mango, Pacha Nne?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru na ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge. Bahati nzuri nilikuwepo Mtwara na tulifanya naye ziara na natambua changamoto hiyo na tayari tulishaipokea, Wizarani tunaifanyia kazi. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati tukiwa tunapata fedha, kwa ajili ya kwenda kutekeleza mradi huu. Ahsante sana.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha ili wananchi wa Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale – Manonga wapate maji ya Ziwa Victoria?
Supplementary Question 4
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria ni mradi muhimu sana kwa sababu, tunatarajia kutatua changamoto ya maji kwa Wakazi wa Rorya, Mji wa Tarime na Tarime DC, ambao ulitarajiwa kukamilika Mwaka 2025. Ninataka tu kujua kwa sasa umefikia asilimia ngapi? Ninakushukuru.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana dada yangu, Mheshimiwa Esther Matiko, kwa kazi nzuri anayoifanya. Mradi huu ambao unaanzia Tarime, Rorya unaenda mpaka Serengeti, Mugumu. Kwa hiyo, tunaamini kabisa kwamba, huu mradi utaenda kusaidia sana katika wilaya kadhaa ambapo wananchi wa pale watapata huduma ya maji safi, lakini tunapotoa takwimu sahihi Mheshimiwa Mbunge anikubalie kwa sababu, ni suala la takwimu na Serikali haitakiwi kutoa takwimu ambazo siyo sahihi. Nimuombe baada ya hapa nilifanyie kazi, halafu nimpatie takwimu halisi kwamba, umefika asilimia ngapi exactly, kwa ajili ya manufaa ya wananchi wake wote. Ahsante sana.
Name
Samweli Xaday Hhayuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hanang'
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:- Je, lini Serikali itatenga fedha ili wananchi wa Kata za Igoweko, Uswaya na Tambalale – Manonga wapate maji ya Ziwa Victoria?
Supplementary Question 5
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini wananchi wa Bassodesh, Mureru na Gijetamohog watapata maji safi na salama bombani, ikiwa visima vimeshachimbwa na mabomba yako site zaidi ya mwaka sasa?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Mhandisi kwa kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi wake na mradi huo ambao tayari hatua ya kwanza tulichimba visima, lakini baadaye pia, tukanunua vifaa, ikiwemo mabomba, matanki na kadhalika. Sasa, hatua ya mwisho ni kuhakikisha kwamba, tunaenda kulaza yale mabomba pia, kutengeneza maeneo ambayo wananchi wanaweza kupata hiyo huduma ya maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge changamoto iliyokuwepo sasa hivi tayari tumeshaifanyia kazi na mabomba hayo yataenda kulazwa, ili yaweze kutoa huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana.