Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 43 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 192 | 2025-04-30 |
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti mimba za utotoni, nchini?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya visababishi vya mimba za utotoni ni pamoja na uelewa mdogo wa watoto kuhusu elimu ya afya ya uzazi na uwajibikaji duni wa wazazi na walezi katika kutunza na kulea watoto kikamilifu. Katika kukabiliana na tatizo hilo, Serikali inatekeleza Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka wa fedha 2024/2025 hadi 2028/2029, ambao moja ya kipaumbele ni kupunguza mimba za utotoni kwa 50% ifikapo Mwaka 2029, inaunda madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule za msingi na sekondari, inawakumbusha wazazi au walezi wajibu wao wa msingi wa kulea na kutunza watoto na imefanya marekebisho ya Sheria ya Elimu na Sheria ya Mtoto kwa kuongeza adhabu kwa wanaowapa watoto mimba, watoto na wazazi wasiotunza na kulea watoto.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved