Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amina Daud Hassan
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti mimba za utotoni, nchini?
Supplementary Question 1
MHE. AMINA DAUD HASSAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Serikali imeamua kuwarejesha wanafunzi waliopata mimba za utotoni shuleni. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwawekea mazingira mazuri ili kuepuka kunyanyapaa?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Amina kwa kujali na kumuunga mkono Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwarejesha watoto waliopata changamoto kwenye masomo yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imeelekeza watoto wote wanaopata changamoto za mimba za utotoni, baada ya kujifungua warudi shuleni. Mheshimiwa Rais akaliona hilo na akaelekeza mikoa yote ya Tanzania zijengwe shule za bweni, ili watoto hawa waweze kunusurika na kuondokana na changamoto za mimba za utotoni na ukatili. Ahsante. (Makofi).
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved