Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 15 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 193 2025-04-30

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:-

Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya, kupitia Halmashauri ya Busokelo, inajulikana kwa jina la Number One – Lugombo, yenye urefu wa kilometa 30. Barabara hii ni ya Wilaya iliyokasimiwa TANROADS kutoka TARURA mwaka 2023. Serikali imepanga katika mwaka wa fedha 2026/2027 kuanza maandalizi ya kuijenga barabara hii kwa kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili ijengwe kwa kiwango cha lami. Kwa sasa, Serikali inaendelea kuifanyia barabara hii matengenezo ya kawaida ili iweze kupitika katika majira yote ya mwaka.