Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 1
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, nitoe pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha kujenga Barabara ya kutoka Katumba – Suma – Mpombo – Isange mpaka Ruangwa kwa kiwango cha lami. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais katika historia hii imeandikwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Barabara hii ya Number One – Ngumburu imefungwa kutokana na mvua nyingi zinazonyesha na hakuna gari wala pikipiki inayopita katika barabara hii. Je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kuhakikisha barabara hii inafunguliwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Barabara kutoka Kandete Mjini – Luteba nayo imefungwa kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika Jimbo hili la Busokelo. Je, Serikali ina mpango gani pia wa kupeleka vifusi, kwa ajili ya kufungua Barabara hii ya Kandete – Luteba? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mwakibete, yote kwa pamoja, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii, kama nilivyosema, imekasimiwa TANROADS na ilikuwa ni barabara ya udongo. Kwa hiyo, tumeshaomba fedha za dharura na katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha, nyingi sana, katika huo ukanda. Nitumie nafasi hii kumwelekeza Meneja wa Mkoa wa Mbeya aende akafanye tathmini ya barabara zote mbili ambazo zimefungwa; na Kwa kuwa, wakandarasi wako jirani waweze kutusaidia kufungua na kama kutakuwa na changamoto inayohitaji nguvu kutoka Wizarani, basi aweze kutoa taarifa haraka, lakini ikiwezekana leo aende, ili akafanye tathmini na barabara hizo zote mbili ziweze kufunguliwa. Ahsante. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 2
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, Kipande cha Barabara kati ya Mbulu – Garbabi hadi Hydom imekuwa na changamoto kubwa sana kwa wananchi katika kipindi hiki cha mvua; na Kwa kuwa, mkandarasi wa Kichina ametekeleza kipande hicho. Je, Serikali inatoa kauli gani kumwagiza yule mkandarasi kwenda kujenga barabara ya kawaida ya wananchi ili wananchi waendelee kupata huduma? Ninakushukuru.
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ziko barabara ambazo zilikuwa ziko na wakandarasi na zikawa zimesimama kwa sababu ya kutokulipa, ama advance payment ama certificate, kwa maana ya hati ambazo walikuwa wanazidai. Ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine kwamba, tayari Serikali imeshaanza kupeleka fedha na mkandarasi huyo aliyemtaja wa Mbulu – Garbabi, tayari ameshapelekewa advance, ameshapelekewa malipo ya certificate, ambayo alikuwa ameomba.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe wito kwa mameneja wote kwamba, pale ambapo pana wakandarasi wajibu wao ni kuhakikisha kwamba, zile barabara zinapitika, ziwe barabara kubwa zile ama za michepuko ili tusikatishe mawasiliano ambayo yapo. Ni wajibu wa wakandarasi na ipo kwenye mikataba yao, ikiwepo na Barabara ya Mbulu – Garbabi. Ahsante.
Name
Nancy Hassan Nyalusi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 3
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kinyanambo – Madibira ni barabara ya kimkakati. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara hii? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara aliyoitaja imeshafanyiwa usanifu. Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Name
Maimuna Salum Mtanda
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Newala Vijijini
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 4
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa nafasi hii. Ni lini Serikali itatenga fedha, kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara ambayo inaunganisha Mkoa wa Mtwara na Lindi kupitia Mtama – Kitangali hadi Newala, kilometa 74? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara aliyoitaja amekuwa anaiulizia mara kwa mara. Ni barabara ambayo tayari tumeshajenga maeneo baadhi korofi kwa vipande vile ambavyo vinasumbua, lakini mpango ni kuijenga barabara hiyo yote kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 5
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara kipande kinachoanzia Itoni hadi Lusitu imekuwa na hali mbaya sana kwa sasa na kusababisha kero kwa wananchi. Je, ni lini Serikali itamaliza majadiliano na mkandarasi, ili aendelee kufanya kazi?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Mkandarasi wa Itoni – Lusitu tayari tumeshamlipa sehemu ya malipo yake. Kwa hiyo, tunamwagiza Meneja wa Mkoa wa Njombe ahakikishe anamsimamia, ili aweze kwenda kazini na ahakikishe kwamba, ile barabara ambayo ilikuwa imekwama maeneo yote anayafungua na wananchi wasipate hiyo changamoto. Ahsante.
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 6
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, Mheshimiwa Rais ameshatoa fedha, kwa ajili ya kilometa 11 za njia mbili Barabara ya Moshi – Arusha, kipande cha Maili Sita mpaka Kiboroloni, Moshi; na Kwa kuwa, TARURA nao wana fedha, kwa ajili ya kutengeneza barabara ya njia mbili kutoka NBC Roundabout mpaka YMCA na tutapata fedha, kwa ajili ya YMCA – KCMC. Je, mko tayari kukaa na TARURA, ili kutengeneza design nzuri ya Roundabout ya YMCA? Ninashukuru sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote taasisi hizi mbili zinashirikiana kwa ukaribu sana, TARURA na TANROADS, kwa sababu, barabara zao zinahusiana sana. Ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na niwape maelekezo watendaji wakuu wa hizi taasisi, kama tupokee ujumbe wa Mheshimiwa Mbunge, wakae na washirikiane. Ikiwezekana, kama una mawazo tukukaribishe ili uweze kutoa mawazo yako nini unafikiri kinaweza kikafanyika kwa ubora zaidi. Ahsante.
Name
Bupe Nelson Mwakang'ata
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 7
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itajenga Barabara ya kutoka Namanyele Mjini – Kipili kwa kiwango cha lami? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, hii barabara tulishakamilisha usanifu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, nina hakika katika bajeti ambayo tutakuja kuisoma hapa pia, itaonekana, kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Je, lini Barabara inayounganisha Jimbo la Busokelo na Mbeya yenye kilometa 28, itajengwa ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kupitia Suma hadi Katumba?
Supplementary Question 8
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Madihani – Busokelo – Kitulo – Busokelo ni barabara ambayo TANROADS mlianza kujenga, lakini imesimama. Ni ipi Kauli ya Serikali kujenga barabara hii, ili ikamilike wananchi wasizunguke Mbeya kuelekea Busokelo, waweze kukatisha?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, eneo hili analolisema ni eneo ambalo lina mvua nyingi na ni la miinuko. Kwa hiyo, wamesimama si kwa sababu hawapo, lakini kwa sababu wanapisha hii hali ya hewa ambayo hata wakijenga leo, barabara yote inaweza kuondolewa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mpango upo na wakandarasi wataendelea kuijenga hiyo barabara. Ahsante.