Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 15 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 194 2025-04-30

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. MASACHE NJELU KASAKA aliuliza:-

Je, lini Selikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kuanzia Makongolosi hadi Mkiwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa yenye urefu wa kilometa 413 ni sehemu ya Barabara ya Mbeya – Lwanjilo – Chunya – Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa yenye urefu wa kilometa 524. Ujenzi wa barabara hii unafanyika kwa awamu, ambapo sehemu ya Mbeya hadi Makongolosi, kilometa 111, ujenzi umekamilika. Sehemu ya Noranga – Itigi, Mlongoji, kilometa 25 ujenzi unaendelea na umefikia 76% na sehemu ya Itigi, Mlongoji – Mkiwa, kilometa 31.57, mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza kazi. Kwa sehemu iliyobaki ya kutoka Makongolosi hadi Noranga, kilometa 356.43 Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuendelea na ujenzi.