Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Anyigulile Jumbe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. MASACHE NJELU KASAKA aliuliza:- Je, lini Selikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kuanzia Makongolosi hadi Mkiwa?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; wananchi wa Chunya na Wanambeya kwa ujumla wangetamani sana kuona barabara hii inaanza kujengwa mara moja na hasa ikianzia upande wa Chunya. Je, Serikali itaanza lini ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kutokea Makongorosi – Lupa – Mkiwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Wilaya ya Chunya haijaunganishwa na Mkoa wa Songwe kwa lami na eneo hilo ni lile linalounganisha Mbalizi na Makongolosi. Ni lini barabara ya kutoka Mbalizi – Makongolosi ikienda mpaka Mkwajuni, itaanza kujengwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge ambaye ameuliza swali kwa niaba ya Mbunge wa Chunya. Tunatambua kama Wizara kwamba sera ni kuunganisha mikoa yote kwa kiwango cha lami; na kati ya barabara kubwa ambazo zimebaki, ambazo pia ni trunk, barabara kuu, ni hii ya Chunya kwenda Itigi na vilevile Barabara ya Chunya kwenda Tabora kupitia Ipole.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuendelea kujenga kwa hatua kulingana na upatikanaji wa fedha ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba mpango wa Serikali ni kutafuta chanzo cha uhakika cha fedha ili barabara hiyo iweze kuunganishwa mikoa Nyanda za Juu Kusini na mikoa ya Kaskazini. Tunaiona kama ni barabara moja muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, kwa swali la pili pia tayari tumeishaanza, tumekwishatangaza kuanzia Mbalizi kwenda Mkwajuni na pia kuanzia Mkwajuni kwenda Mbalizi ili kuanza kujenga kipande hicho kwa lami. Kwa kutambua umuhimu huo Mheshimiwa Mbunge atakubaliana na nami kwamba tulikuwa na changamoto ya madaraja mawili makubwa ambayo yalikuwa yanasumbua, madaraja ya Lupa – Tinga na Binti Manyanga ambapo tayari Mheshimiwa Samia amekwishatoa fedha kwa ajili ya kuyajenga hayo madaraja ili kusiwe na mkwamo tena. Ahsante. (Makofi)

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. MASACHE NJELU KASAKA aliuliza:- Je, lini Selikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kuanzia Makongolosi hadi Mkiwa?

Supplementary Question 2

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami kilometa 22 za Barabara ya Isyonje – Kikondo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii inakwenda hadi Makete. Tumekwishaanza upande wa Makete na katika mwaka huu tunategemea fedha ili tuanze pia upande wa Mbeya kwenda Makete ili tuweze kukamilisha hicho kipande chote. Ahsante. (Makofi)

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. MASACHE NJELU KASAKA aliuliza:- Je, lini Selikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kuanzia Makongolosi hadi Mkiwa?

Supplementary Question 3

MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Mtwara Mjini kuna barabara ambayo ilijengwa na TANROAD kutoka keep left hadi bandarini na barabara ile iliharibiwa na Kiwanda cha Dangote ambao walikuwa wanapitisha mitambo mikubwa. Tukalalamika na Serikali wakasema kwamba watazungumza na watu wa Dangote ili warekebishe barabara ile. Je, ni lini watakuja kuirekebisha barabara ile?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimwelekeze Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mtwara. Pia nitawasiliana na Mheshimiwa Mbunge ili tujue changamoto iliyokuwepo. Tuliijenga barabara hiyo na Dangote ni kwa nini kama aliamuliwa ajenge na hajajenga ili tuweze kutoa majibu ya uhakika. Ahsante.

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. MASACHE NJELU KASAKA aliuliza:- Je, lini Selikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kuanzia Makongolosi hadi Mkiwa?

Supplementary Question 4

MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Barabara ya kutoka Lizaboni – Londoni – Lupapila hadi Litapwasi itajengwa kwa kiwango cha lami? Ninakushukuru. (Makofi)
MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, kutoka Lizaboni kwenda Londoni – Lupapila hadi Litapwasi kwa kiwango cha lami.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, hii barabara kwanza tunakamilisha usanifu. Tulitambua kwamba kuna shida kubwa sana ya kuvuka mto mitoni. Tunavyoongea sasa hivi hilo daraja ambalo ndilo lilikuwa changamoto kubwa tunalijenga kuanzia sasa na wakandarasi wako site. Kwanza tukamilishe hiyo ili ipitike halafu tuanze mipango ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. ahsante.