Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 15 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 195 2025-04-30

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka magari kwenye vituo vya Polisi Mkoani Mbeya?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Jeshi la Polisi hugawa vitendea kazi kama magari kwa uwiano sawa katika mikoa yote hapa nchini. Katika ugawaji huo pia huzingatia ukubwa wa eneo, wingi wa watu, shughuli za kiuchumi, matukio ya uhalifu na wingi wa makosa ya usalama barabarani. Katika mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 Mkoa wa Mbeya umepata magari mapya 12, hivyo kufanya kuwa na jumla ya magari 43 yanayofanya kazi. Serikali itaendelea kutenga fedha toka kwenye bajeti kila mwaka kwa ajili ya kununulia vitendea kazi kwa ajili ya Jeshi la Polisi ikiwemo magari. Ahsante.