Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 178 2025-02-11

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Chumba cha Upasuaji katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilipokea jumla shilingi bilioni 2.94 na kujenga majengo 12 ya hospitali ya wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali itatenga shilingi milioni 265 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo. Ahsante.