Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Anna Richard Lupembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Chumba cha Upasuaji katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo?
Supplementary Question 1
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Natoa shukrani zangu kwa majibu mazuri ya Serikali. Pia, naomba niipongeze Serikali kwa kazi kubwa, kwa majengo yote hayo 12 yaliyojengwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa wananchi wanapata shida sana hususani akinamama wajawazito, hawana mahali pa upasuaji wakati wa kujifungua. Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kujenga jengo dogo la dharura kuhakikisha akinamama wale waweze kupona maisha yao?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kwa kuwa Serikali imefanya kazi kubwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo na hatuna kabisa theatre ya magonjwa mbalimbali, wananchi wanatumia gharama kubwa kwenda katika maeneo mbalimbali hususani mikoa mbalimbali. Je, Serikali haioni kufanya dharura ya kujenga theatre katika Hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, Hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo haina jengo la upasuaji na Serikali kwa kulitambua hilo katika bajeti ambayo sasa tumeanza mchakato wake ya mwaka 2025/2026 itatenga shilingi milioni 265 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, hoja hiyo imeshapokelewa na Serikali na tayari imeshaingizwa kwenye mpango na tutakwenda kujenga jengo la upasuaji mwaka ujao wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kweli kwamba tuna utaratibu wa kujenga majengo ya upasuaji na wodi ya akinamama pamoja; lakini pia tunayo mipango ya kujenga majengo ya upasuaji pekee yake kwa ajili ya magonjwa ya wanaume, wanawake na wagonjwa wengine. Katika mpango wa Serikali, tumeanza na utaratibu wa kukamilisha majengo ya upasuaji ya akinamama na wodi zao, na baadaye tutajenga majengo ya upasuaji general, pamoja na wodi za wanaume, wanawake na watoto. Hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa mama Lupembe kwamba, mpango huo upo na tutahakikisha kwamba tunajenga majengo hayo ili tupate huduma bora katika Wilaya ya Nsimbo. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved