Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 179 2025-02-11

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaipatia ufumbuzi changamoto ya upungufu wa vifaa tiba na watumishi kwenye baadhi ya vituo vya afya nchini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kuajiri na kuwapangia vituo vya kazi wataalam wa kada mbalimbali za afya katika ngazi ya msingi kote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024, Serikali ilitoa shilingi bilioni 187.37 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali za halmashauri. Aidha, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi bilioni 66.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na hadi kufikia Disemba, 2024 jumla ya shilingi bilioni 43.13 zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imeendelea kuajiri wataalam wa kada za afya ambapo katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2023/2024, jumla ya wataalam wa kada za afya 25,917 wameajiriwa na kupangiwa vituo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira na kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini. Ahsante.