Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 180 2025-02-11

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itakipatia Gari la Wagonjwa Kituo cha Afya cha Upuge – Uyui?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuimarisha huduma za rufaa za wagonjwa, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2024/2025 Serikali imenunua na kusambaza magari 382 ya kubebea wagonjwa kwenye halmashauri kwa kuzingatia mahitaji, ambapo kila jimbo limepokea angalau gari moja la kubebea wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ilipokea magari matatu ya kubebea wagonjwa ambayo yamepangwa kutoa huduma katika Hospitali ya Wilaya, Kituo cha Afya Igalula na Loya. Aidha, Kituo cha Afya Upuge - Uyui kina gari la wagojwa ambalo ni chakavu hali inayopelekea kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mpango wa manunuzi wa magari ya wagonjwa na kuyapeleka kwenye vituo vyenye uhitaji zaidi kikiwemo Kituo cha Afya cha Upuge – Uyui, ahsante.