Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza:- Je, lini Serikali itakipatia Gari la Wagonjwa Kituo cha Afya cha Upuge – Uyui?

Supplementary Question 1

MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Swali la kwanza; Kituo cha Afya cha Upuge hakijapata kuwa na gari la wagonjwa, isipokuwa gari bovu la halmashauri, ambalo walienda wakali-pack pale na kituo kile kinahudumia kata tatu. Je, Serikali sasa iko tayari kutambua kituo kile hakina gari la wagonjwa wala hakijawahi kupata gari la wagonjwa linalofanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa vile Kituo cha Afya cha Upuge kinahudumia watu zaidi ya 30,000 na hakina huduma ya X-ray wala Ultrasound, isipokuwa zinapatikana katika hospitali ya wilaya ambayo ipo kilometa 15 hadi 20 kutoka pale. Je, Serikali iko tayari kupeleka gari la wagonjwa katika mgao unaoendelea? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Almas Maige amekuwa akifuatilia mara kadhaa kuhusiana na uhitaji wa gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Upuge na mara kadhaa tumekaa naye na tumekubaliana kuhusu suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tu, kwamba tayari tumeingiza kwenye orodha ya vipaumbele, vituo vya afya vipaumbele, ambavyo vitapelekewa magari ya wagonjwa, ni pamoja na Kituo cha Afya cha Upuge, hatua za utekelezaji zinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Serikali imeweka mpango wa kukamilisha majengo ya huduma na kuweka vifaa tiba muhimu ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Nimhakikishie kwamba, katika kipindi cha miaka hii mitatu, Serikali imenunua Digital X-Ray zaidi ya 250 na kusambaza kwenye vituo vya afya na hospitali za halmashauri. Kituo hicho alichokitaja Mheshimiwa Mbunge kitapewa kipaumbele ili kipate mashine ya Digital X-Ray ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. Ahsante sana.