Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 181 2025-02-11

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:-

Je, Serikali inatofautishaje Kaya Maskini Vijijini na Mijini katika kuwaunganishia umeme nchini?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TANESCO na EWURA imeweka mwongozo wa gharama za kuunganisha umeme kwa wateja, ambapo gharama hizo hutofautiana kulingana na hali ya eneo. Kulingana na mwongozo huo, maeneo yanayotambuliwa kama miji na vijiji miji, gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 320,960 na kwa maeneo ya vijiji gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 27,000, ahsante.