Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, Serikali inatofautishaje Kaya Maskini Vijijini na Mijini katika kuwaunganishia umeme nchini?

Supplementary Question 1

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninashukuru Serikali kwa majibu iliyotoa, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali haioni kutofautisha maskini hawa wa mijini na vijiji miji ni kutowapatia haki maskini ile fursa ya kujiinua kiuchumi kwa kupata nishati ya umeme?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kwa kuwa maskini hawa katika pande zote za vijijini na mijini pia wanatambuliwa katika mpango wa Serikali unaoitwa TASAF na fedha nyingi zinatumika katika kuwalipa. Je, Serikali haioni sasa kupitia TASAF iendelee kuwapa ile hali na haki ya kutumia shilingi 27,000 kuwaunganishia umeme hawa wanaoishi kwenye miji? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge na naomba niyajibu kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya kupeleka umeme inatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha kwa category tofauti tofauti. Miradi ambayo tunapeleka kwa 27,000, ni miradi ambayo imekuwa categorized kwa ajili ya miradi ya vijijini, ni miradi ambayo Serikali inaweka ruzuku ili hawa wananchi waweze kupata umeme kwa gharama nafuu kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa maeneo ya miji na vijiji miji tuna miradi mingine ya peri-urban, namna ambavyo tunawasaidia wananchi ambao uwezo wao wa kuunganisha umeme ni kidogo ni kupitia kupeleka miradi kwa karibu. Kwa mfano maeneo ya miji, tunapeleka miradi ya peri-urban na wanaunganishiwa kwa shilingi 27,000, lakini ni lazima aunganishe katika kipindi ambacho miradi hii inatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile hata kwenye maeneo ya miji tunapeleka miradi hii, hususani kwa maeneo ya pembezoni ili wananchi na wenyewe waweze kupata umeme kwa gharama ambayo ni himilivu kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, hii miradi tunaitekeleza kwa aina tofauti tofauti kulingana na maeneo ili kuendelea kumpa ahueni mwananchi katika kuunganisha umeme. Ahsante.