Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 182 2025-02-11

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itafungua rasmi na kuanza kutumika Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lililojengwa katika eneo la Ndea Wilayani Mwanga?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufunguzi wa Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa Mkomazi lililojengwa katika eneo la Karamba – Ndea, Wilayani Mwanga ulipangwa kufanyika tarehe 27 Disemba, 2024 pindi matengenezo ya kuiboresha barabara ya kuingilia kwenye lango hilo kwa kiwango cha changarawe kukamilika mwezi Novemba, 2024.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kufuatia mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha hifadhini na kwenye maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Taifa Mkomazi, matengenezo ya kuiboresha barabara kwa kiwango cha changarawe ili iweze kutumika kwa shughuli za utalii yalishindikana kukamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa matengenezo ya barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.5 kutoka Lango la Ndea hadi mpakani mwa Hifadhi ya Taifa Mkomazi upande wa Wilaya ya Mwanga, yanaendelea. Kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari, 2025 na mara baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo Wizara imepanga ufunguzi rasmi wa Lango la Karamba – Ndea ufanyike mwezi Machi, 2025.